loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Afungwa maisha kwa kubaka mgonjwa kikongwe

Raia wa Kenya aishiye Texas nchini Marekani Anthony Nyakeo, hivi karibuni amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka bibi kizee wa miaka 74 ambaye alikuwa mgonjwa.

Mahakama imeeleza kuwa kitendo hicho kilifanyika Januari 2018 katika kituo cha afya cha Woodridge Health and Rehabilitation ambapo Nyakeo alikuwa muuguzi na bibi huyo akiwa mgonjwa.

“Baada ya tukio hilo, wauguzi wengine wa kituo hicho walikuta damu kwenye nguo za ndani za kikongwe huyo, na baadaye vipimo vya DNA vilithibitisha Nyakeo kufanya kitendo hicho kilichomsababishia majeraha makubwa kwenye sehemu za siri bibi huyo,” imeeleza mahakama.

Hatahivyo bibi huyo alifariki miezi kadhaa baada ya tukio hilo, lakini kesi iliendelea kusikilizwa.

Hukumu hii inakuja miezi michache baada ya Mkenya mwingine jijini humo Dallas kukutwa na hatia ya kuua vikongwe wanawake 11.

RAIS wa Urusi, Vladimir ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Post your comments