loader
Picha

Uchaguzi serikali za mitaa Nov 24

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ametangaza kuwa, uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika Novemba 24 mwaka huu.

Amesema Mtumba, Dodoma kuwa kura zitapigwa kuanzia saa mbili asubuhi na mwisho wa kupiga kura itakuwa saa 10 jioni.

Ametaja nafasi zitakazogombewa kuwa ni Mwenyekiti wa Kitongoji, Mwenyekiti wa Mtaa, wajumbe wa kamati za mitaa, wenyeviti wa vijiji, na wajumbe wa halmashauri ya kijiji, wenyeviti wa vitongoji.

Waziri Jafo amesema, wagombea wanapaswa kuwa wanachama wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu na wanatakiwa kudhaminiwa na vyama hivyo.

Amesema uandikishaji wapigakura na uandaaji wa orodha yao utaanza siku 47 kabla ya uchaguzi na utafanyika kwa siku saba.

Jafo amesema, uandikishaji huo utafanyika kwenye majengo ya umma na ambako hakuna majengo hayo utafanyika kwenye sehemu ambayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atakuwa amekubaliana na viongozi wa vyama vya siasa.

Amesema vituo vya kujiandikisha vitakuwa katika ngazi za vitongoji na mitaa.

Waziri Jafo amesema, yeyote anayekusudia kugombea anapaswa kuchukua fomu ya uteuzi siku zisizopungua 26 kabla ya siku ya uchaguzi.

MAWAZIRI wa Sekta wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi wa nchi zilizo ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi