loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali iendelee kuboresha mazingira ya biashara

SERIKALI imejipanga kuongeza ushirikiano wake na sekta binafsi ili kuondoa kero na vikwazo na kuweka mazingira bora ya biashara kuvutia uwekezaji wa ndani na pia kutoka nje ya nchi.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema hayo wakati akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA mwaka huu.

Alitoa wito kwa chama hicho kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza katika kufanya biashara.

Tumeguswa na ujumbe wa Waziri Mkuu, Majaliwa kwa wafanyabiashara na kuungana naye kuwataka wafuate taratibu na miongozo.

Ni kwa kufanya hivyo, wafanyabiashara hao wataboresha mazingira ya biashara ya mikoa na wilaya, ambapo serikali imeshaweka mwongozo wa mabaraza hayo ambayo TCCIA ni sekretarieti.

Tunaomba wafanyabiashara kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi mikubwa ambayo inatekelezwa na serikali hasa ya miundombinu ya reli ya kisasa, umeme bwawa la Nyerere, bomba la mafuta la Tanga-Hoima na ndege.

Tunakubaliana na Waziri Mkuu kuwa, huu ni wakati muafaka wafanyabiashara hao kubaini maeneo maalum ambayo TCCIA itaendelea kutoa mchango mkubwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II). Ni katika kutekeleza mpango huo wa pili, sekta binafsi inatarajiwa kupewa nafasi zaidi katika uboreshaji biashara mbalimbali wanazofanya.

Hivyo, tunaomba wafanyabiashara wote nchini kuhakikisha wanatumia vema fursa hizo kwa lengo la kuongeza uzalishaji mali na kuinua pato la taifa. Wakifanya hivyo, itasaidia kupanua wigo wa uzalishaji mali na mwisho wa siku kukuza pia uchumi wetu na kukidhi malengo ya mpango huo.

Tunaipongeza serikali kutambua ushirikiano mzuri wa TCCIA na taasisi za Umoja wa Mataifa (UN) za UNDP, Unido, FAO, UNV, Unesco, ILO, ITC na wadau wengine wa maendeleo.

Tunaamini ushirikiano wa taasisi hizo na serikali utarahisisha utekelezaji wa mpango wa ASDP II na hivyo kuzaa matunda haraka kama ambavyo serikali imepanga kupata mafanikio.

Kwa taasisi nyingine na wadau wa maendeleo tunaomba watoe ushirikiano kwa serikali na TCCIA ili kufanikisha ajenda ya kuifanya nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Tunaipongeza serikali kwa kukubali kuendelea kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara wote nchini ikilenga kupata mafanikio makubwa. Tunaomba utaratibu huo uendelee katika maeneo mengine ili kuongeza kasi ya maendeleo na mwisho tufanikiwe kama nchi.

KUANZIA leo hadi Jumapili wiki hii jijini Dodoma, Chama Cha ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi