loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuunge mkono wakimbizi Burundi kurudi kwao

KUANZIA Oktoba mwaka huu wakimbizi 2,000 wa Burundi, watarejeshwa nyumbani kwao kila wiki, kutokana na kuimarika usalama.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alisema juzi kuwa urejeshaji huo wa wakimbizi, utafanyika baada ya makubaliano ya serikali ya Tanzania na Burundi, yaliyofikiwa hivi karibuni.

Awali serikali hizo mbili, zilikubaliana idadi hiyo ya wakimbizi watakaorejeshwa, lakini kwa sababu mbalimbali idadi ya wakimbizi ambao walikuwa wakirejeshwa, ilikuwa watu 300.

Wakimbizi hao ni walioko kwenye makambi mbalimbali mkoani Kigoma. Kutokana na awali zoezi la kuwarejesha kusuasua, Lugola alisema sasa watarejeshwa, hata kama hakuna msaada wa taasisi za kimataifa, ikiwemo Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Tunaungana na wananchi wengine, kuzipongeza serikali za Tanzania na Burundi, kukubaliana kuwarejesha wakimbizi wa Burundi kwao. Tunaomba hatua hii iungwe mkono na jumuiya ya kimataifa, kwani inalenga kuleta amani Burundi.

Tunaomba wakimbizi wanaohusika, wajitokeze kuomba kurudi kwao, wakaijenge nchi yao hasa wakati huu serikali yao inapochukua hatua za kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali.

Tunaungana na Waziri Lugola, kukemea wote wanaokwamisha wakimbizi hao kurejea makwao, kwa nia ya kuhujumu juhudi za serikali ya Tanzania na Burundi, kurejesha utulivu huko.

Madai yaliyotolewa na Waziri Lugola kuwa baadhi ya maofisa wa taasisi za kimataifa, ambazo zinahusika na wakimbizi, wanadaiwa kuwazuia baadhi wanaotaka kuandikishwa kurejea kwao, hazipaswi kupuuzwa kamwe.

Ni kwa msingi huo, tunasema iko haja kwa jumuiya ya kimataifa, kuunga mkono hatua hii nzuri inayochukuliwa na nchi hizi, kuhakikisha wakimbizi wanarudi Burundi kujenga nchi yao. Hatua yoyote inayoonekana kuhujumu au kudhoofisha malengo mazuri ya kuwarudisha kwao wakimbizi, inapaswa kushughulikiwa.

Si vizuri hata kidogo wakimbizi wa Burundi, kuzuiwa kurudi kwao, wakati wengi wameonesha utayari kutokana na hali ya amani na usalama, kurejea nchini mwao sasa.

Wakiwa kwao Burundi, wakimbizi hao watakuwa na uhakika wa maeneo mengi ya kulima na kufanya shughuli nyingine za kiuchumi kwa uhuru zaidi na nafasi kubwa.

Wakiwa nchini wamekuwa wakikosa fursa hiyo kutokana na kukaa kambini, ambako hakuna maeneo makubwa wakimbizi kulima au kufuga na hivyo kuwarudisha nyuma maendeleo yao.

KUANZIA leo hadi Jumapili wiki hii jijini Dodoma, Chama Cha ...

foto
Mwandishi: Mhariri

1 Comments

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi