loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Viola Davis ‘kuwa’ Michelle Obama tamthilia ‘First Ladies’

Mwigizaji wa nchini Marekani Viola Davis anatarajiwa kuigiza kama mke wa Rais Mstaafu wa nchini humo Michelle Obama katika tamthilia mpya ya ‘First Ladies’.

Mshindi huyo wa tuzo ya Oscar pia atakuwa moja ya watayarishaji wakuu wa tamthilia hiyo ambayo itazungumzia maisha binafsi na ya kisiasa ya wake wa marais wa Marekani katika historia ya nchi hiyo.

Msimu wa kwanza wa tamthilia hiyo utazungumzia maisha ya Eleanor Roosevelt, mke wa Rais mstaafu Franklin Roosevelt na Gerald Ford mke wa Rais mstaafu Gerald Ford.

Rais Mstaafu wa nchi hiyo Barack Obama na mkewe Michelle waliingia makubaliano na kampuni ya Netflix mwaka 2018 ili kushiriki kwenye uzalishaji wa filamu fupi na makala.

Baada ya kusaini mkataba huo Obama alisema “filamu na makala hizi zitagusia masuala ya ubaguzi wa rangi, matabaka, demokrasia, haki za kiraia na mengineyo na matumaini yetu ni kwamba hazitaburudisha tu hadhira bali zitaelimisha, zitatuunganisha na kutupa hamasa.”

foto
Mwandishi: JANETH MESOMAPYA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi