loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongera serikali kujenga vivuko Mwanza, Geita

SERIKALI imetoa Sh bilioni 7.3 kwa ajili ya ujenzi wa vivuko viwili vya Bugorola - Ukara wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza na Chato -Nkome mkoani Geita kuondoa changamoto ya usafiri wa maji iliyopo kwa wakazi wa maeneo hayo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Japhet Maselle amesema hayo juzi alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya uwekaji msingi wa ujenzi wa vivuko hivyo.

Alisema mjini Mwanza kuwa kivuko cha Bugorola - Ukara kinajengwa kwa Sh bilioni 4.2 na cha Chato -Nkome kwa Sh bilioni 3.1, fedha za serikali zinazotokana na mapato ya ndani.

Tumepokea habari za kujengwa kwa vivuko hivyo kwa furaha na tunaungana na wakazi wa maeneo hayo kuishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuwaondolea kero hiyo. Wakazi wa maeneo hayo kwa muda mrefu wamekuwa na changamoto ya usafiri wao binafsi na mazao au bidhaa zao kutokana na maeneo yao kuwa visiwa visivyofikika kirahisi.

Ndio maana tunasema, uamuzi wa serikali ya Rais John Magufuli kutoa fedha zote hizo kujenga vivuko kwa ajili ya wakazi wa maeneo hayo, unastahili pongezi za kila mwananchi.

Unastahili kupongezwa kwa sababu umekuja wakati muafaka hasa ukizingatia kuwa wakazi wa maeneo hayo wengine wamekutwa na maafa kama yaliyotokea Ukara mwaka jana ya kuzama kivuko cha Mv Nyerere kilichoua watu wengi.

Ni wazi, kujengwa kwa vivuko vipya kwa ajili ya visiwa hivyo kutawahakikishia wananchi wanaoishi huko, usafiri salama na wa uhakika hivyo kuchochea shughuli zaidi za uchumi na maendeleo yaliyokwamishwa na kukosa usafiri.

Tunaomba serikali iendelee kuviangalia kwa jicho la huruma, visiwa vingine vilivyo maeneo ya pembezoni ili kuwarahisishia maisha watu.

Tunajua serikali ina nia njema na watu wake ndio maana inazidi kuchukua hatua mbalimbali kuboresha maisha yao kwa kuanzisha miradi mingi ya umeme ya Mto Rufiji, maji, reli ya kisasa ya SGR, kununua ndege na mengineyo kama hayo.

Tumeshuhudia nia njema hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaac Kamwelwe kuzindua ujenzi wa kivuko kwa ajili ya wakazi wa Mafia -Nyamisati wilayani Mafia, Pwani.

Wakazi wa Mafia, moja ya visiwa vikubwa vya Bahari ya Hindi wamekuwa na shida ya usafiri pia kwa muda mrefu na hivyo kutaabika ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha na mali zao nyingi.

Ni matarajio yetu, hatua hizi za serikali ya awamu ya tano, zitaleta unafuu wa maisha yao baada ya mwaka mmoja au miwili kulingana na muda ambao wakandarasi watajenga vivuko.

Tunaomba wananchi wa maeneo hayo na pia mengine ambayo hayajabahatika kutatuliwa matatizo yao kuiunga mkono serikali iwasaidie.

TANZANIA itakuwa na ugeni mkubwa wa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi