loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtoto mlemavu anaomba baskeli asome awe mwalimu

BINTI mlemavu mwenye umri wa miaka 10, Sophia Yona mkazi wa Kata ya Membe Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma aliyekuwa akifungiwa ndani na kukosa fursa ya kwenda shule anasema, sasa anaamini ndoto zake za kusoma na kuwa mwalimu zitatimia.

Licha ya kufungiwa ndani na kukosa fursa ya kwenda shule, amejua kusoma na kuandika kutokana na kufundishwa na watoto wenzake.

Akizungumza namna walivyomwibua binti huyo, mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Msingi Membe, Elisha Michael anasema amekuwa akifundisha watoto wa shule ya awali, lakini alikuwa akishangazwa na baadhi ya watoto hao kuwa na uelewa mkubwa darasani.

Anasema baadhi ya watoto walikuwa wakifahamu kusoma na kuandika vizuri na hata somo la Hisabati, lakini hakuweza kubaini walikuwa wakifundishwa na nani.

Michael anasema katika mizunguko yake hapo kijijini, alibaini uwepo wa mtoto mlemavu anayesema anatamani kuwa mwalimu, lakini hajaanza masomo.

“Nilifuatilia na hatimaye kufika kwa wazazi wa mtoto huyo ambao walisema, walishindwa kumpeleka shule kutokana na ulemavu alio nao.”

“Nilijaribu kutafuta uwezekano wa kumsaidia Sophia nikakutana na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Membe, Adolph Alfred; tulipomtembelea mtoto huyo, alisema anataka kusoma na nilipomuuliza anapenda nini, akasema anapenda kusoma na anatamani siku moja atembee kama mdogo wake,” anasema.

Hata hivyo mwalimu huyo anabainisha kuwa, baadaye aligundua kuwa, wanafunzi waliokuwa wakifundishwa na Sophia walikuwa wakifanya vizuri darasani.

Anasema: “Nikabaini zaidi kuwa, kumbe Sophia alikuwa akifundishwa na watoto wengine rafiki zake akiwa hapo nyumbani kwao na ndipo baada ya kuelewa, naye akawa anafundisha watoto wa chekechea hapohapo nyumbani kwao…”

Mwalimu huyo wa sekondari ya Membe, Adolf, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Social Action For Association and Development (SAFAAD); anasema wamekuwa wakishughulika na walemavu pamoja na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

“Nilipomuona mtoto huyo nikasema bora ningemfahamu mapema kwani licha ya mazingira anayoishi alijitahidi kuhakikisha anajua kusoma na kuandika,” anasema. Anasema utaratibu wa kuwajulisha viongozi wa kata hiyo akiwemo diwani ulifanyika na katika Ofisi ya Idara ya Maendeleo ya Jamii nao walisema kuwa watafuatilia jambo hilo.

Diwani wa Kata ya Membe, George Malima anasema alipopigiwa simu na mwalimu alikuwa hafahamu chochote juu ya uwepo wa mtoto huyo mwenye ulemavu na wala hafahamu chochote kuhusu mtoto kama huyo kuwepo katika kata yake. “Nilikaa na Sophia na wazazi wake tukampa karatasi na kalamu alikuwa akijua kusoma na kuandika na alifahamu kupitia kwa wanafunzi waliokuwa wakitoka shuleni na kwenda kumfundisha

wala hamkumbuki,” anasema. Anasema wamekuwa pia wakijielekeza katika kujenga vyoo kwa ajili ya wanafunzi kujisitiri hususani wasichana wanapokuwa katika hedhi na pia wanatoa elimu kwa jamii kuchangishana fedha ili kuhakikisha watoto wanapata chakula cha mchana shuleni.

Anafafanua kwamba njaa, mbali na kuwafanya watoto washindwe kufuatilia masomo vyema, inachangia pia urahisi wa wanaume wapuuzi kuwarubuni mabinti kwa kuwanunulia chakula.

Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilayani Kishapu, Rahel Madundo, anasema kampeni yao katika kuwafanya wanafunzi kubaki na sare muda wote imesaidia idadi ya mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika baadhi ya maeneo kupungua.

Halima Salum na Makoye Marko, wakazi wa kijiji cha Negezi, kata ya Ukenyenge wanakiri kwa nyakati tofauti kushiriki katika mkutano ulioazimia wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari kushinda na sare zao popote wanapokwenda.

“Tumeona hatua hiyo inaweza kusaidia kuwaogopesha wanaopenda kuwatongoza wanafunzi na kwa kweli wanapokuwa hawana sare huonekana ni wakubwa,” anasema Marko. Mwenyekiti wa kijiji cha Negezi, kata ya Ukenyenge, John Mayala anasema:

“Tumeona hatua hii ya kuhakikisha wanafunzi wanavaa sare muda wote ikisaidia kupunguza mimba. Mwaka huu msichana aliyepata mimba ni mmoja tu katika kijiji hiki. Nawashukuru pia wazazi kuongeza juhudi za kulinda mabinti zao.”

Diwani wa kata ya Ukenyenge, Anderson Mandia, anasema hatua ya kuwataka wanafunzi wavae sare ilitokana na ukweli kwamba wasichana wengi walikuwa wakirubuniwa na wafanyabiashara wa minada ambao wanawaona ni wakubwa wanapokwenda huko bila sare.

“Tulipitisha hatua hii kwenye mkutano wa hadhara kwa kushirikiana na vituo vya taarifa na maarifa vilivyoibuliwa na mtandano wa jinsia Tanzania (TGNP) ambavyo vinatusaidia pia katika kupambana pia na ukatili wa kijinsia katika jamii yetu,” anasema.

Ofisa Elimu Sekondari wa halmashauri ya Kishapu, David Mashauri anasema suala la kujenga hosteli pia lina changamoto zake akitolea mfano shule ya sekondari Mipa ambako baada ya hosteli kujengwa baadhi ya wazazi waligoma kupeleka watoto wao kuishi huko kwa kisingizio kwamba hawawezi kuwahudumia.

Mashauri anasema kwa mwaka jana idadi ya mimba katika wilaya hiyo ilikuwa 56 na kwamba lengo la kujengwa kwa hosteli ni kupunguza wimbi la mimba kwa wanafunzi.

“Ujenzi wa hosteli unaendelea kwa shule za sekondari ili kuondoa changamoto ya mwanafunzi kutembea umbali mrefu ambao unachangia baadhi ya wanafunzi wa kike kupata mimba lakini mtoto anapokuwa katika hosteli mzazi atatakiwa kuwajibika kwa mahitaji ya mtoto wake na hapo ndipo kunatokea changamoto,” anasema ofisa elimu huyo.

Ofisa maendeleo ya jamii, Joseph Swalala, anasema pamoja na jitihada za serikali kuja na sera ya elimu bure, suala la mimba kwa wanafunzi limeendelea kuwa changamoto katika wilaya Kishapu licha ya baadhi ya kata kufanya vizuri.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba anakiri kwamba baadhi ya wazazi wanakataa watoto wao wa kike kukaa hospitali kwa kuhofia gharama ya mahitaji lakini anasema hali hiyo inachangia hali ya mimba kutopungua.

Anahimiza kila kijiji au kata kupitia viongozi wao kuja na mikakati mizuri ya kupambana na mimba mashuleni kwa kushirikiana na wazazi.

walikuwa wakiondoka, yeye akawa anaanza kuwafundisha watoto wa chekechea. Kwa kweli hili ni jambo lililonigusa sana,” anasema.

Anasema taasisi yake imekuwa ikishughulika na masuala ya watoto na anatamani kuona watoto wenye ulemavu wanapewa fursa ya kupata elimu na siyo kufungiwa ndani kama ilivyokuwa kwa Sophia.

Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Wilaya ya Chamwino, Sophia Swai, anasema baada ya kupata taarifa za uwepo wa mtoto huyo aliwasiliana na Idara ya Eimu waliosema mtoto huyo anaweza kuanza darasani la tatu kwenye madarasa ya Memkwa (Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa) ili mwakani asajiliwe darasani la nne.

“Tunatakiwa kuangalia jinsi atakwenda shule na kuangalia ndoto ya Sophia. Wazazi waache kuficha watoto walemavu nyumbani maana sasa elimu ni bure, hakuna kisingizio,” anasema.

Mtoto Sophia anasema alifahamu kusoma na kuandika kupitia kwa watoto wenzake, waliokuwa wakitoka shule na kupitia kwao kucheza, lakini akawa anawaomba wamfundishe wanayojifunza shuleni.

“Sijaenda shule kwa vile siwezi kutembea… Naomba nipatiwe baiskeli niwe naendea shuleni kusoma ili nije kuwa mwalimu,” anasema Sophia.

Mama wa Sophia, Erodia Malonga anasema mtoto huyo alizaliwa mwaka 2008 katika Zahanati ya Kijiji cha Membe. “Alipozaliwa alikuwa na tatizo la kutetemeka lakini sikuelewa tatizo ni nini,” anasema mama huyo.

Anazidi kufahamisha kuwa, walimpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Misheni ya Mlali iliyopo wilayani Kongwa na wakaambiwa kuwa, hakuwepo daktari wa kumshughulikia, hivyo, wakaamua kurudia nyumbani. Baba mzazi wa Sophia, Hamisi Yona anasema mtoto huyo alizaliwa akiwa na ulemavu. Anasisitiza: “Naomba tu msaada ili apate baiskeli na matibabu.”

Anaongeza: “Nimehangaika naye sana wakati akiwa mdogo, nakumbuka nilienda Mlali kila tukienda tunamkosa daktari; tunaambiwa daktari wa kushughulikia tatizo lake yupo nje ya nchi mpaka atakaporudi.

Baadae, nikaamua kuuliza kwa kutumia simu tu, lakini kila tukipiga simu tunaambiwa daktari hajarudi, tukakata tamaa kabisa,” anasema.

Hata hivyo, anasema hawakuridhika hivyo, waliamua kuendelea kupambana hadi walipofanikiwa kumfikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Katika hospitali hiyo mzee huyo anasema, mwanawe alifanyiwa vipimo na kutakiwa kuwa anampeleka katika mazoezi mara mbili kwa wiki.

Anasema kuwa hata hivyo, kutokana na gharama ikiwamo nauli kumshinda na familia yake, walifanikiwa kumudu kumpeleka katika mazoezi tiba hayo kwa wiki mbili pekee.

Kwa msingi huo anasema hawakuwa na namna nyingine ya kumsaidia Sophia zaidi ya kubaki naye nyumbani. Tayari binti huyo amepata cheti cha kuzaliwa na atapatiwa bima ya afya kisha kupelekwa kupata uchunguzi wa afya yake ili kubaini chanzo cha ulemavu wake.

Idara ya Maendeleo ya Jamii imeandika barua kwenda Ofisi ya Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa ajili ya kuomba kiti cha magurudumu maarufu wheel chair ili kumsaidia mtoto huyo mlemavu mwenye kipaji cha ajabu.

“Tukipata bima ya afya atakwenda kuchunguzwa ili kubaini chanzo cha tatizo lake kwani anaonekana yuko dhaifu sana,” anasema Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Chamwino, Sophia Swai.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga anasema ni wajibu wa mzazi kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya kupata elimu.

Anawataka wazazi kuacha kuwaficha ndani watoto wenye ulemavu kwani wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine wasio na ulemavu.

Sera ya Taifa ya Mtoto ya Mwaka 2007 pamoja na sheria zake ikiwamo Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, zinaweka bayana haki za watoto, wajibu wa watoto, wajibu wa wazazi, walezi, wajibu wa taasisi za serikali, wanasiasa, viongozi wa dini, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na wananchi.

Wadau kwa nyakati tofauti, wanaomba mtu au taasisi yoyote itakayoguswa, kuchangia kufanikisha masomo kwa mtoto huyu anayeonesha uwezo mkubwa.

Kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi