loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ndumbaro- Mahakama A. Kusini imetenda haki

Mahakama Kuu ya Gauteng imeamuru kuachiwa kwa ndege ya Serikali ya Tanzania inayosimamiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa imezuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini tangu Agosti 24, 2019.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Damas Ndumbaro amesema nchini humo kuwa, Mahakama hiyo imekubali hoja zote za mawakili wa Tanzania hivyo Serikali imeshinda kesi na ndege imeruhusiwa kuondolewa uwanjani hapo.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Mahakama hiyo pia imeamuru mlalamikaji alipe gharama za kesi.

Dk Ndumbaro amesema, Mahakama imesema, kama Steyn ana hoja nyingine anaweza kufungua kesi Tanzania, na kwamba, amri ya Mahakama ya Tanzania inaweza ikatekelezwa na Mahakama za Tanzania na si Mahakama za Afrika Kusini.

Amesema, mlalamikaji jana alifungua kesi nyingine kupinga hukumu iliyosomwa leo hivyo wanashangaa alijuaje hukumu hiyo ingekuwa dhidi yake hadi akakata rufaa kabla ya kusomwa hukumu leo.

"Kwa hiyo sisi tunaishukuru sana Mahakama ya Afrika Kusini kwa kutenda haki lakini tunawashukuru zaidi Watanzania ambao wameunga mkono juhudi zetu za kuinasua ndege hii kutoka huku Afrika Kusini"amesema Dk Ndumbaro.

KAMPUNI ya Chai Bora imesema licha ya kuwepo kwa ugonjwa ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

1 Comments

  • avatar
    faustin cheyo
    06/09/2019

    mko vizuri sana kwa kutupatia yanayo jili nawakubari

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi