loader
Picha

Mwanaume matatani kwa kupika nyama ya mbwa

JESHI la Polisi katika jimbo la Tharaka Nithi, nchini Kenya linamshikilia mwanaume mmoja kwa kuchinja mbwa na kumpika kwa madai ya alikuwa ana njaa.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Munene alikamatwa na polisi hao jana, Alhamisi, akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Karimba akiwa anachemsha sehemu ya nyama hiyo ya mbwa kwenye sufuria, huku kiasi kingine akiwa amekihifadhi ndani.

Alipoulizwa sababu za kufanya hivyo, Munene alisema kwamba alikuwa ana njaa kwani hakuwa amepata chakula kwa kipindi cha siku tatu.

“Nilikuwa naandaa mboga hii ili niile na ugali,” alieleza mwanaume huyo wakati akijaribu kujitetea kwa polisi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Haki za Wanyama nchini humo, mtuhumiwa anaweza kupigwa faini ya hadi Sh 45,000/- au kifungo cha miezi isiyozidi mitatu kwa kosa la ukatili dhidi ya wanyama.

SERIKALI ya Uganda imesema itatuma Dola za Marekani milioni 60 ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi