loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuendelee kushawishi wananchi bima za matibabu

KUTOKANA na kuzidi kupanda kwa gharama za matibabu, juhudi zinazofanywa na serikali kushawishi wananchi wajiunge na bima kupunguza makali ya matibabu ni za kupigiwa makofi na kushangiliwa.

Ipo mikoa mingi ambayo imeamua kwa makusudi mazima kuboresha mifumo ya bima ya jamii ili iweze kusaidia wananchi wake kwa maeneo husika.

Juhudi zote hizo tunasema ni za kupigiwa makofi na kushangiliwa kwa sababu kuna gharama kubwa katika matibabu kwa kutoa fedha taslimu hasa ununuzi wa dawa husika au katika vipimo au kumuona daktari.

Kwa kukosa bima ya afya wananchi wengi maskini wanyonge hujikuta wanakwama kusaidia familia zao wakati wakiwa msambweni.

Ndio kusema kampeni zinazofanywa na baadhi ya mikoa nchini zinastahili kueplekwa kila mkoa ili wananchi wengi waweze kujiingiza katika bima baada ya mavuno au kwa wale wanaofuga basi washawishike kuuza sehemu ya mifugo yao kuweza kulipia bima.

Ndio kusema serikali inawapowataka wananchi wake kujiunga na mfumo wa bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini inatakiwa kupigiwa mstari wa utekelezaji na kila mtu.

Hili lisibaki kuwa suala la wanasiasa pekee au la watabibu bali wananchi wote na hasa taasisi zisizo za kiserikali (NGO) katika miradi yao kuhakikisha kwamba wanahi miza washiriki kuhakikisha wanaingia katika mifumo hiyo ya matibabu kila wanapopata nafasi.

Tungeshauri kwa taasisi hizo hata kama zinakwenda mradi fulani wasisahau kuunganisha miradi hiyo na afya za wananchi wanaowatumikia, ili hata kile wanachokieleza kiweze kuwakaa.

Hakika mwili dhaifu kiafya hauwezi kusikiliza mambo ambayo NGO hizo inataka wananchi waelewe.

Ni kweli hatuwezi kuzalisha mali wala kutoa huduma kama hatuna uhakika wa maisha ya matibabu na kwa namna ya ajabu kabisa ugonjwa huja siku au wakati ambapo mtu ana shida nyingi za kiuchumi.

Kutokana na ukweli huo ni vyema wananchi wahamasike kuingia katika mifumo ya bima ili kuwawezesha kupata huduma za afya kwa gharama nafuu sana.

Upo msemo kwamba kidole kimoja hakivunji chawa, msemo huu ni murua katika maisha yetu kwa kuangalia ukweli kuwa bila na nguvu za pamoja hatuwezi kukabiliana na maradhi ambayo mara zote kama si kawaida hujitokeza wakati wa mazingira magumu.

Na kwa kuwa sisi hatuna mazoea ya kupima afya, wananchi wengi huwa tunaumwa magonjwa ghafla baada ya kukaa nayo muda mwingi na kukomaa kiasi ya kwamba matibabu yake huwa mtihani mkubwa.

Hakika wakiwa ndani ya mfumo wa bima watakuwa na uhakika wa kupata dawa kwa makundi yote kwa muda wote kwani fedha zao ndio zitachangia pia kuhakikisha kwamba zahanati au hospitali haikosi dawa na vifaa tiba.

KUMEKUWAPO na habari za kufurahisha kuhusu mashirika zaidi ya ndege ...

foto
Mwandishi: Tahariri,

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi