loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ubunifu watakiwa upatikanaji wa maji

HUDUMA ya maji ni kati ya mambo muhimu katika maisha ya kila siku pia ikiwa ni kati ya viungo muhimu katika upatikanaji wa Tanzania ya viwanda. Maji ndio kila kitu kuanzia katika uzalishaji wa mali hadi utumiaji wake na katika masuala ya usafi.

Ifahamike kuwa kati ya mambo muhimu kuhusiana na maji ni suala zima la ubora, wingi pamoja na upatikanaji wake. Wadau wamekuwa wakishirikiana na serikali katika kupigania upatikanaji wa maji safi na salama.

Ili kufanikisha ushiriki kikamilifu wa sekta binafsi katika kufanikisha azma hiyo ni wazi kuwa mbinu bunifu na shirikishi zinapaswa kuzingatiwa ili kufanikisha malengo hayo.

Ninaungana na harakati za mradi wa Bits and Bytes ambao umeshindanisha vijana tisa kupata watano washindi ambao mawazo yao yatachukuliwa na kusimamiwa na mradi huo, mawazo ambayo yanatoa suluhisho kuhusiana na nini kifanyike katika kuhakikisha maji yanapatikana.

Mawazo kama haya ndio yanaweza kuwa chachu itakayohakikisha Tanzania inakuwa salama katika hekaheka za kuwa na maji safi na salama.

Shughuli za kibinadamu ni kati ya mambo yanayoathiri uhakika wa maji na hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa katika kukabiliana na hali hiyo.

Aidha kunatakiwa kuwa na mikakati kabambe ya udhibiti upotevu wa maji ili kila tone litumike kwa makusudi yaliyopangwa. Ndio maana naona ipo haja ya ubunifu kupelekwa kila mahali ili maji yawe bidhaa endelevu kwa wananchi wa Tanzania.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: NA EVANCE NG’INGO

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi