loader
Picha

Timu ya riadha kuagwa Arusha Septemba 23

TIMU ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya 17 ya dunia inatarajia kuagwa jijini Arusha Septemba 23, imeelezwa. Tanzania katika mashindano hayo ya Dunia yatakayofanyika Qatar mwaka huu kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 6, itapeleka wanariadha wanne tu, watatu wakiume na mmoja wakike, wote wakishiriki mbio za marathoni.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday alisema jana kuwa, timu hiyo ambayo itakuwa na wanariadha wanne na viongozi watatu wa RT, itaagwa jijini Arusha tayari kwa safari siku inayofuata.

Wanariadha hao na muda wao bora katika mabano ni Augustino Sulle (2:07:44), Alphonce Simbu (2:08:27) na Stephano Huche (2:12:24) wakati mwanamke pekee katika msafara huo ni Failuna Abdi (2:27:36).

Gidabuday alisema mwanariadha mwingine aliyefuzu kushiriki mashindano hayo ya dunia ni Ezekiel Ngimba 2:13:34, lakini kutokana na kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Riadha (IAAF) kuruhusu nchi kuwa na wachezaji watatu katika mchezo mmoja, Ngimba ameenguliwa sababu ya muda wake kutokuwa mzuri.

Gidabuday alisema kuwa hivi karibuni watamtangaza mgeni rasmi atakayekabidhi bendera timu hiyo, ambayo watu wengine wanaotarajia kuwemo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa RT, William Kallaghe, ambaye anamuwakilisha Rais wa shirikisho hilo, Antony Mtaka.

Wengine wanaotarajia kuwemo katika msafara huo ni Gidabuday mwenyewe na makamu wa pili wa RT, Dk Hamad Ndee. Timu hiyo kwa mujibu wa Gidabuday, itaondoka mafungu mawili, ambapo kundi la kwanza, ambalo litakuwa na Kallaghe na Failuna wataondoka mara baada ya kuagwa wakati fungu jingine litaondoka Oktoba 2.

Alisema Failuna anawahi kwa kuwa mbio yake itachezwa siku ya ufunguzi wa mashindano hayo Septemba 27 wakati Kallaghe anawahi sababu ya Mkutano Mkuu wa IAAF, ambao utakuwa pia na Uchaguzi Mkuu.

Mkutano Mkuu wa 52 wa uchaguzi utafanyika Septemba 25 na 26 na utawachagua Rais wa IAAF, makamu wanne wa rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji.

TIMU za Ligi Kuu Tanzania Bara zimegomea mfumo mpya unaotarajiwa ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi