loader
Picha

Kocha Msoma alia na hujuma

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Malindi, Abdulghani Msoma amesema kumekuwepo hujuma za makusudi anazofanyiwa, ambazo zinarejesha nyuma juhudi zake za ufundis haji.

Msoma aliyasema hayo kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na mipango yake kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika na timu ya Almisri.

Malindi ambayo imesonga hatua ya pili ya kimakundi baada ya kuwatoa Mogadishu City, ambapo sasa mchezo wao wa awali wa hatua ya pili wataanzia nyumbani September 13 mwaka huu.

Alisema kuwa wamekuwa wakijitahidi kujipanga, lakini tatizo kubwa liliopo ni kufanyiwa hujuma. Alitaja moja ya hujuma, ambayo amefanyiwa ni kutokana na kuidhinishwa mchezaji wake Ibrahim Bata katika klabu ya KMKM, ambaye alikuwa mchezaji wa timu yao.

Alifahamisha kwamba kutokana na kitendo hicho, kikosi chake kimeparaganyika katika sehemu ya ulinzi kutokana na kuondokewa na mchezaji huyo, lakini tayari wachezaji walishakaa sawa kimazoezi kwenye safu hiyo.

“Kuondoka kwake tumeparaganyika katika ulinzi sasa kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuwaweka sawa”, alisema. Hatahivyo, alisema kuwa wapo kwenye kujibadilisha na wiki moja hiyo iliyobakia unaweza kuwasaidia kukava.

KOCHA wa timu ya soka ya wanawake ya Tanzania chini ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi