loader
Picha

Mikoa minne kuchuana baiskeli Arusha

MIKOA minne imethibitusha kushiriki mashindano ya wazi ya baiskeli yaliyopangwa kufanyika Septemba 14 jijini hapa. Waendesha baiskeli 120 kutoka maeneo mbalimbali watapepetana katika michuano hiyo ilioandaliwa na Kampuni ya RexLex Cycling ya Arusha.

Akizungumza kuelekea mashindano hayo, mratibu wa mbio hizo mchungaji Joel Senny alisema mpaka sasa maandalizi yanakwenda vyema na tayari washiriki wameanza kujiandikisha kutoka mikoa ya Dar es Salaa, Simiyu, Shinyanga, Manyara na Arusha watashiriki.

Alisema waendesha baiskeli wamekuwa na umoja sana na hii inaashiria kuujenga mchezo huo na kuwa mmoja wa michezo inayopendwa sana hapa nchini.

Alisema mashindano hayo yatahusisha kilomita 80 kwa wanaume, kilomita 60 kwa wanawake, kilomita 60 kwa wazee na kilomita 30 kwa watakaokimbia kwa ajili ya kujifurahisha tu.

“Tunashukuru tumepata ushirikiano mkubwa kutoka vyombo vya usalama, ambapo Jeshi la Polisi wametupa kibali na kutuhakikishia usalama katika mbio hizo na pia tunatarajia mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro,” alisema Senny.

Alizitaja zawadi zitakazo tolewa kuwa ni mshindi wa kwanza kwa kilomita 80 atajinyakulia sh 500,000, mshindi wa pili 300,000 na mshindi wa tatu atapata 200,000 na kusema zawadi zitaboreshwa kwa washindi wengine wa nafasi tofauti.

Kwa wanawake kilomita 60 na wazee kilomita 60 mshindi atazawadiwa sh 150,000 mshindi wa pili atapata 100,000 na watatu 50,000 kila mmoja.

Kwa upande wake, Habiba Mathias ambaye ni mwendesha baiskeli kwa wanawake alisema amejiandaa vyema kushindana na kuwasihi wanawake wajitokeze kuupenda mchezo huo.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi