loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Stars gumzo bungeni

BUNGE limeipongeza Timu ya Soka ya Taifa, Taifa Stars kwa ushindi ilioupata dhidi ya Timu ya Taifa ya Burundi, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia Qatar 2022 uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.

Spika wa Bunge, Job Ndugai alitoa pongezi hizo kwa niaba ya wabunge wote baada ya kukamilika kwa kipindi cha maswali na majibu jana.

Katika mchezo huo Taifa Stars iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti penati 3-0 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 120, matokeo yalikuwa kama hayo pia katika mechi ya kwanza iliyochezwa Bujumbura mapema mwa wiki iliyopita.

Ushindi huo unaifanya Stars kufuzu hatua ya makundi ya kuwania fainali hizo ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya soka ya Tanzania.

Spika Ndugai alisema molari iliyooneshwa na wachezaji wa Taifa Stars katika mchezo wa juzi ilikuwa ya hali ya juu na kuitaka kuongeza molari zaidi kwa michezo ya hatua ya makundi ili izidi kusonga mbele zaidi na hatimaye ifuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.

Alisema Bunge limefurahishwa na ushindi huo ambapo alisema umeipa heshima kubwa Tanzania na kuitangaza katika ulimwengu wa mchezo wa soka.

Kabla ya mchezo wa juzi, Bunge kupitia kwa Mwenyekiti wake Mussa Azzan Zungu waliitabiria ushindi Taifa Stars, utabiri ambao ulitimia kwa Stars kushinda na kusonga mbele.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi