loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC- Huwezi kuvutia wawekezaji bila TIC

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema huwezi kuandaa kongamano la uwekezaji lenye maana bila kukihusisha Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Ndikilo ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipoongoza ujumbe wa serikali ya Mkoa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuzungumza na menejimenti ya TIC.

“Sasa unapoona kuna kongamano la uwekezaji TIC anaingia moja kwa moja na mimi kwa maoni yangu huwa nasema kongamano hili la uwekezaji na TIC mahusiano yake kwa maoni yangu ni kama maji na samaki, inseparable (huwezi kuvitenganisha), eeh hakuna kongamano la uwekezaji bila TIC. Sisi tunaona kwamba ili kongamano hili liweze kuwa na maana, lifanikiwe, lazima awe sehemu, kabisa kabisa ya shughuli hii kubwa ”amesema.

Mhandisi Ndikilo amesema, wamekwenda TIC ili washauriwe namna ya kufanikisha kongamano hilo Oktoba tatu mwaka huu ili liwe na matokeo chanya ndani na nje ya nchi.

Amesema, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) wataandaa maonesho ya viwanda yanayotarajiwa kuhusisha viwanda visivyopungua 400 kutoka mikoa ya Tanga, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani.

“Wana uzoefu mkubwa, ndani na nje ya nchi nao tumewahusisha ili tuone sasa kwamba maonesho haya yanakuwa na vionjo vizuri ili kuweza ku-attract (kuvutia) watu wengi zaidi ili waweze kuona bidhaa zinazozalishwa katika Mkoa wetu wa Pwani na wananchi wajue lakini pia hata na wenye viwanda wenyewe waweze kupata biashara katika bidhaa hizo”amesema

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ametoa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi