loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hakuna kama Pwani viwanda vipya

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema ujenzi wa viwanda mkoani humo si jambo la siasa, vipo, anayetaka aende kuviona.

Amesema jijini Dar es Salaam kuwa, tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani mkoa huo ndio unaoongoza kwa ujenzi wa viwanda vipya vikubwa na vya kati.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, katika miaka minne ya uongozi wa Serikali hiyo Pwani imejenga viwanda si chini ya 100 vya ukubwa huo.

“Vidogo na vidogo sana ni kwenye zaidi ya mia tano sasa ndio maana huwa tunawa-challenge sisi, huwa tunawa-challenge wenzetu kwamba tunadhani kama tukifanya inventory ya viwanda vipya ndani ya Serikali ya Awamu ya Tano Mkoa wa Pwani lazima watapa tabu sana kuweza kutupata” amesema Ndikilo.

Amesema, hadi sasa Mkoa wa Pwani una jumla ya viwanda 1,192 vikiwemo vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo sana.

Ametaja miongoni mwa maeneo yenye viwanda kuwa ni Rufiji, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Kibaha na Chalinze

“Kwenye ajenda ya viwanda ya Mheshimiwa Dk John Pombe Joseph Magufuli aingie madarakani, vikubwa na vya kati not less than 100 vipya ambavyo havikuwapo na ndio maana tunawa-challenge sisi tunawaambia kwamba tunajenga viwanda njooni muone”amesema.

Amesema, Oktoba Mosi hadi saba mwaka huu kutakuwa na Maonesho ya Pili ya Viwanda Mkoa wa Pwani na pia Oktoba tatu mkoa huo utatekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kuwa na Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji.

“Alitoa maagizo kwamba kila mkoa uandae muongozo wa uwekezaji, uutangaze ndani na nje ya nchi.”amesema.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ametoa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi