loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkakati kilimo cha korosho kuungwa mkono

SERIKALI imesema ipo tayari kuunga mkono mkakati wa kilimo cha korosho wilayani Kongwa mkoani Dodoma Kauli hiyo ilitolewa juzi na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Biashara wilayani humo, mbele ya Mwenyekiti wa baraza hilo na Mkuu wa Wilaya hiyo Deogratias Ndejembi.

Mkutano huo ulifanyika katika Mamlaka ya Mji mdogo Kibaigwa wilayani humo ambapo ajenda kuu ilikuwa ni kilimo cha korosho na zao la chakula la mtama.

Mkutano huo uliojadili mkakati wa kilimo cha korosho ulihudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Taifa, Mangile Malegesi na Wataalamu kutoka kituo cha utafiti wa Kilimo Naliendele kutoka Lindi na wananchi wawakilishi kutoka kata 22.

Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kilimo wilayani humo, Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika, Jackson Shija alisema hadi mwaka huu wilaya hiyo ina wakulima 301 wenye mashamba ekari 4,253 yenye mikorosho 65,408, Alisema zao hilo linasaidia kuongeza kipato cha mkulima, kurudisha uoto wa asili na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema changamoto kubwa katika kutekeleza mkakati wa kilimo hicho ni pamoja na duka la pembejeo za korosho kufunguliwa mbali ambako ni wilaya ya jirani ya Mpwapwa, pamoja na ufugaji holela. Alizitaka serikali za vijiji kuhakikisha zinasimamia matumizi bora ya ardhi.

Pia, wameomba TARI Naliendele ione uwezekano wa kuleta wataalamu wa kilimo hicho kwa ajili ya elimu zaidi kwa wakulima. Katika mkutano huo, Bashe alitoa maagizo manne na makubaliano ya muda wa utekelezaji wa maagizo hayo.

Maagizo hayo ni pamoja na bodi ya korosho kuhakikisha kituo cha pembejeo kinahamishwa haraka kutoka Mpwapwa kwenda Kongwa na bodi hiyo kuanzisha kwa kituo cha kuhudumia na kusapoti wakulima zao hilo.

Maagizo mengine mawili ni halmashauri hiyo kushirikiana na bodi kutengeneza ramani ya vituo vya uzalishaji mbegu kutokana na mtawanyiko wa wakulima katika maeneo ili kurahisisha wakulima kufikiwa na mbegu kirahisi.

Ofisa Kilimo wa Kongwa Shija ahakikishe wakulima wa zao hilo wote wanasajiliwa na kupewa namba zao za usajili na kuwe na kompyuta maalumu ya kanzidata ya wakulima wa korosho

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi