loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Polisi 5, askari JWTZ kizimbani wizi wa mafuta

ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) na Askari Polisi watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya wizi wa mafuta ya ndege mali ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na kutakatisha fedha zaidi ya Sh milioni nne.

Washitakiwa hao ni Koplo Shwahiba (38), Sajini Ally Chibwana (47) wa JWTZ, Konstebo Elidaima Paranjo (38), Konstebo Simon (28), Konstebo Dickson na Konstebo Hamza ambao walifikishwa mahakamani hapo jana wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka akisaidiana na Saada Mohammed alidai washitakiwa wote hao wakiwa ni watumishi wa umma walikiuka maadili ya kazi zao na kupanga genge la uhalifu na kuiba lita 2,180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh 4,647,760.

Alidai Julai 30, mwaka huu huko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washitakiwa waliiba lita 2,180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh 4,647,760 mali ya ATCL.

Inadaiwa siku na mahali hapo washitakiwa wote waliiba mafuta hayo na kutakatisha kiasi hicho cha Sh milioni 4.6 huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi kinyume cha sheria.

Washitakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi Mahakama Kuu au pale Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) atakapotoa kibali cha mahakama hiyo kusikiliza.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi