loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rufiji kuwa chanzo cha maji Dar

MAMLAKA ya Maji Safi na Taka Dar es Salaam na Pwani (Dawasa) ipo kwenye mchakato wa kutumia maji ya Mto Rufi ji kama chanzo kingine kitakachowezesha mikoa inayohudumia kuwa na maji ya uhakika.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na ujumbe wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, uliomtembelea ofisini kwake.

Ndikilo aliongozana na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers (TSN), pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kwa ajili ya kuelezea maonesho ya viwanda na kongamano la fursa za uwekezaji litakalofanyika mwezi ujao mkoani kwake.

“Tumetumia fursa ya Bwawa la Rufiji linalojengwa na sisi tutajenga mtambo mkubwa wa maji kutoka Rufiji. Tumeshaunda kamati ya kuanza mchakato, tumeshawasiliana na wadau wetu Tanesco ambao ndiyo wenye bwawa,” alisema.

Luhemeja alisema wamewasiliana pia na mkandarasi wa bwawa hilo na Wakala wa Barabara (Tanroads) kwa ajili ya suala hilo.

Alisema wameanza mchakato katika hatua za mwanzo na mwakani watawasilisha hoja kwenye bodi kwa ajili ya kupata kibali kisha upembuzi yakinifu ufanyike na kazi ianze.

Alisema uwezo wa Dawasa ni mkubwa hivyo mtambo utajengwa kwa takribani Sh bilioni 200 ambazo ni fedha za ndani na mradi utaanza Julai, mwakani na utatumia miaka mitatu kabla ya kukamilika.

“Sasa tutakuwa na maji ya uhakika kutoka Ruvu Juu, Ruvu Chini na Rufiji,” alisema. Luhemeja alisema Dawasa imeamua kuondoa shida ya maji Dar es Salaam na Pwani kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya mamilioni ya shilingi, miongoni mwake ni mradi wa Sh bilioni tano utakaozalisha maji lita 280 kwa saa na kuhudumia maeneo ya kutoka Mkuranga mjini hadi Mbagala, Dar es Salaam na kazi hiyo itakamilika Aprili mwakani.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi