loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchungaji wa wake wengi alipa faini kukwepa jela

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh milioni tano, Mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza na wenzake.

Washitakiwa wengine waliohukumiwa ni Esther Sebuyange na Kendewa Ruth ambao ni wake wa mchungaji huyo pamoja na Samwel Samy waliotiwa hatiani katika mashitaka mawili likiwemo kuishi nchini bila kibali.

Akisoma adhabu hiyo jana, Hakimu Mkazi Agustina Mbando alisema Mchungaji Chirhuza anayekabiliwa na mashitaka mawili ya kuishi nchini bila kibali na kuendesha shughuli za uchungaji bila kibali, anatakiwa kulipa faini ya Sh milioni moja kwa kila kosa au kwenda jela mwaka mmoja.

Pia alisema kwa washitakiwa wengine ambao wanakabiliwa na mashitaka ya kuishi nchini bila kibali, watatakiwa kulipa faini ya Sh milioni moja kila mmoja au kwenda jela mwaka mmoja.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Godfrey Nwijo aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa washitakiwa hao ili iwe fundisho kwa wengine.

Mchungaji Chirhuza aliiomba mahakama isimpe adhabu kali kwa sababu kazi aliyokuwa akiifanya ni ya kuitumikia jamii na sio biashara.

Wake wa mchungaji huyo waliiomba mahakama isiwape adhabu kali kwa sababu wana watoto wadogo wanaohitaji upendo wa mama.

Wakisomewa maelezo ya awali, Wakili Nwijo alidaiwa Septemba 2, mwaka huu eneo la Salasala Kilimahewa, Dar es Salaam, Mchungaji huyo na wenzake walibainika kuishi nchini bila kibali.

Pia ilidaiwa kuwa katika tarehe hiyo, mchungaji huyo pekee alibainika kujihusisha na kazi za kanisa akiwa hana kibali cha kuishi nchini.

Ilidaiwa kuwa Septemba 3, mwaka huu, washitakiwa hao walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Walikiri maelezo hayo na maelezo ya onyo yaliyotolewa kama kielelezo.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi