loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Saba wafa ajalini wakienda mnadani, 18 wajeruhiwa

WATU saba wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa wilayani Simanjiro, mkoani Manyara baada ya gari walilokuwa wakisafi ria kwenda mnadani kuacha njia na kupinduka.

Akithibitisha kutokea ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga, jana alisema ilitokea juzi jioni katika barabara ya Arusha – Kiteto maeneo ya kijiji cha Namalulu, kata ya Nabelela, wilayani Simanjiro.

Alisema gari lenye namba za usajili T. 870 AHG aina ya Mitsubishi Fuso iliyokuwa ikiendeshwa na mtu aliyetambulika kwa jina moja la Rashid lililokuwa likitokea Kwa Mrombo jijini Arusha, liliacha barabara na kupinduka na kusababisha vifo vya watu saba na wengine kujeruhiwa.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari kumshinda dereva kutokana na eneo hilo la Namalulu kuwa ni barabara ya vumbi na inakona nyingi na milima hivyo kumshinda dereva na kwenda korongoni na kupinduka.

“Gari hili lilikuwa likiendeshwa na mtu aliyefahamika kwa jina moja tu la Rashidi, lilikuwa limebeba abiria pamoja na bidhaa mbalimbali ambazo zilikuwa zikauzwe mnadani,” alisema Kamanda Senga.

Alisema waliofariki papo hapo walikuwa watano, lakini baadaye walifariki wengine wawili wakati wakipatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Orkesment pamoja na majeruhi 18.

Miili yote ya marehemu imehifadhiwa katika Zahanati ya Orkesment na iliyotambuliwa ni ya Leapa Olekaraa (31), Aloyce Temba (32) mkazi wa Arusha, Moses Mgonja (31) mkazi wa Rombo, Kilimanjaro, Germana Gerard (36) mkazi wa Arusha na Anna Miles (46) mkazi wa Sanya Juu, Hai, huku wawili waliofariki hospitali majina yao yakishindwa kutambuliwa na mpaka jana asubuhi miili iliyotambuliwa ni mitatu na mingine minne haijatambuliwa.

“Juhudi za kumpata mtuhumiwa zinaendelea kwa sababu alitoroka baada ya tukio, lakini nina uhakika mpaka jioni atakuwa amepatikana kama sio mchana kwa sababu mmiliki wa gari anatafutwa na akipatikana tuweze kupata taarifa za huyo dereva aweze kutiwa nguvuni kujibu tuhuma zinazomkabili,” alisema.

Kamanda Senga alionya kuwa taarifa siku zote kuwa magari ya minadani na magari ya mizigo sio ya abiria kisheria, hivyo hayaruhusiwi kupakia abiria kwa usalama wa watu.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Babati

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi