loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yatuma salamu Zesco

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga ni kama wamewasha taa kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Zesco United ya Zambia baada ya kumaliza ziara yao ya Mwanza kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Toto Africans kwenye uwanja wa Nyamagana Mwanza jana.

Mchezo huo ulikuwa wa pili wa kirafiki baada ya ule dhidi ya Pamba kutoka sare ya bao 1-1 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujiimarisha kabla ya kuwavaa Zesco Jumamosi.

Nyota wa mchezo huo ni David Molinga aliyefunga mabao mawili na lingine likifungwa Abdulaziz Makame. Pia, katika mchezo wa kwanza wa Pamba Molinga ndiye aliyefunga bao la kusawazisha kwa Yanga.

Molinga aliyekuwa akibezwa baada ya kufanya vibaya katika baadhi ya michezo iliyopita ya kujipima nguvu na wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting alifunga mabao hayo yote mawili ya jana kwa kichwa dakika ya 36 na 40 huku Makame akifunga dakika ya 47.

Baada ya michezo hiyo ni wazi sasa huenda Kocha Mkuu Mwinyi Zahera akawa amepata mwanga wa muunganiko wa kikosi chake kwa ajili ya mchezo ujao wa kimataifa.

Yanga inatarajiwa kutua Dar es Salaam leo kujiandaa na mchezo huo muhimu kwao kutafuta ushindi kwenye uwanja wa nyumbani ili kutengeneza mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi.

Mbali na Yanga itakayokuwa na mchezo wa kimataifa, pia, Azam FC itacheza Jumapili dhidi ya Triangle ya Zimbabwe katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi