loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

AUSSEMS AHOFIA MECHI NA MTIBWA

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Aussems (pichani) ametoa sababu tatu zitakazochangia mchezo wa keshokutwa dhidi ya Mtibwa Sugar kuwa mgumu.

Mchezo huo wa Ligi Kuu utakaochezwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute. Aussems alisema sababu ya kwanza ni kutokuwa na uhakika wa kumtumia nahodha wake John Bocco aliyeumia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya UD Songo, licha ya kuanza mazoezi mepesi.

Aidha, kocha huyo Mbelgiji pia alisema kikosi chake kitamkosa mshambuliaji wake Mnyarwanda Meddier Kagere aliyeko kwenye majukumu ya kimataifa na timu yake ya Taifa, Amavubi.

Alisema, sababu nyingine ya mechi hiyo kuwa ngumu, ni wapinzani wao kupoteza mechi ya kwanza kwa mabao 3-1 dhidi ya Lipuli hivyo watataka kupata pointi dhidi yao.

“Sababu hizo ndio zinafanya mchezo huo kuwa mgumu kwetu, pamoja na kikosi changu kuanza vizuri lakini bado tunahitaji ushindi kwenye mchezo huo hivyo maandalizi tunayoendelea kufanyika Simba ilishinda mabao 3-1 katika mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya JKT Tanzania.

“Siwezi kumtegemea Kagere kwa sasa kwakuwa yupo kwenye kutimiza majukumu ya timu ya taifa sijajua atafika akiwa fiti au la, hivyo kwa sasa najaribu kuwatengeneza mbadala kwa ajili ya mchezo unaokuja kuhakikisha tunapata ushindi kulinda morali tuliyopata kwenye mchezo uliopita,” alisema.

Alisema pamoja na sababu hiyo timu yake inakikosi kipana hivyo malengo ni kufanya vizuri na kutetea taji lao ili warejee kwenye michuano ya kimataifa.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi