loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kagere mchezaji bora Agosti

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa mwaka 2019/20 wa Agosti, huku Salum Mayanga wa Ruvu Shooting akichaguliwa kocha bora wa mwezi huo.

Kagere na Mayanga walitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzao walioingia nao fainali, katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF.

Kwa mwezi huo kila timu ilicheza mchezo mmoja, ambapo Kagere aliiongoza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania, huku mshambuliaji huyo raia wa Rwanda akifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Kagere aliwashinda Lucas Kikoti wa Namungo FC aliyefunga pia mabao mawili kwa timu yake katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Ndanda na Seif Karihe wa Lipuli aliyeiongoza timu yake kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo alitoa mchango mkubwa katika mchezo huo ikiwa ni pamoja na kufunga bao moja.

Kagere na Karihe hawakupata kadi yoyote, wakati Kikoti alipata kadi ya njano. Kwa upande wa Mayanga aliwashinda Mecky Maxime wa Kagera Sugar na Hitimana Thiery wa Namungo, ambapo aliiongoza Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Yanga.

Maxime aliiongoza pia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Biashara United, huku Hitimana ambaye aliipandisha daraja Namungo FC na kucheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, akiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Ndanda FC.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi