loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli- Nape bado mdogo nimemsamehe

MBUNGE wa Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli baada ya kuhusika kwake katika mazungumzo yasiyofaa dhidi ya Rais.

Nape alikutana na Rais Magufuli jana Ikulu jijini Dar es Salaam. Tayari wabunge wengine wawili ambao ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja nao walimuomba msamaha Rais Magufuli kwa kosa kama hilo, wiki iliyopita na wote wamesamehewa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, katika mazungumzo yake kwa Rais Magufuli, mbunge huyo ambaye alishwahi kuwa waziri katika serikali ya awamu ya tanoi alimshukuru Rais kwa kukubali kukutana naye na kumsikiliza.

Pia alimshukuru kwa kumsamehe kwa makosa aliyoyafanya baada ya kuvuja kwa sauti za mawasiliano yake na wanasiasa wengine wakimsema Rais Magufuli.

“Kwa hiyo baada ya kupata fursa nimekuja nimemuona, na mle ambamo nilimkosea kama baba yangu nimeongea naye na baba amenielewa, ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri ambao nitaufanyia kazi na naamini baada ya hapa mambo yatakwenda vizuri, na kwa kweli kwa dhati ya moyo wangu nimshukuru sana sana, amenipa fursa kubwa, ndefu na ameongea maneno mengi kwangu na ushauri wake nimeuchukua,” alisema Nape.

Kuhusu maendeleo, mbunge huyo alimpongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa inayofanywa na serikali.

Rais Magufuli alisema Nape amekuwa akiomba kukutana naye mara nyingi na tangu siku nyingi kupitia kwa watu mbalimbali wakiwemo wasaidizi wake, viongozi wastaafu na viongozi wa CCM, na kwamba baada ya kukutana naye na kumuomba radhi ameamua kumsahehe.

Rais Magufuli alimtaka mbunge huyo kwenda kufanya kazi za kuhudumia wananchi wa jimbo lake la Mtama na kukitumikia vyema chama chake cha CCM.

“Yote nimesamehe, huyu bado ni kijana mdogo, ana matarajio makubwa katika maisha yake, mimi nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu kwanza ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu na tumefundishwa katika maandiko yote tusamehe saba mara sabini,” alisema.

Aliongeza kuwa “Kwa hiyo nimemsamehe na Mungu amsaidie katika shughuli zake akafanye kazi zake vizuri, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama, akawatumikie wananchi wa jimbo lake vizuri, mimi nimemsamehe, labda kama yeye atakengeuka hiyo itakuwa ni juu yake, lakini mimi kutoka moyoni mwangu nimeshamsamehe na nimemsaheme kweli. Nape nenda ukafanye kazi, Mungu akujaalie,” alisisitiza Rais Magufuli.

Septemba 3, mwaka huu wakati akizungumza na watalaamu wa ujenzi, Rais Magufuli alieleza kuwa amewasamehe wabunge Ngeleja na January ambao nao wanadaiwa kuhusika kutokana na sauti zinazodaiwa zao kusambaa mitandaoni wakiwa wanamzungumzia vibaya rais huyo.

“Nilijiuliza... kila siku mimi huwa naomba msamaha kwa Mungu, kwa ile sala ya “tusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe wengine”, nikaona hawa waliokuja kuniomba msamaha nisipowasamehe nitabaki na maumivu makubwa hivyo nikaamua kuwasamehe...,” amesema.

Aliongeza kuwa “Hawa waliokuja kuniomba msamaha na kutoa kweli katika dhamira yao ni January Makamba na William Ngeleja.” Katika msamaha huo, January aliliambia gazeti hili anamshukuru Rais kwa msamaha huo.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi