loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gofu Lugalo yawatunuku waandishi HabariLeo

KLABU ya Jeshi ya Gofu ya Lugalo imewatunuku vyeti waandishi wa habari za michezo wa gazeti la HabariLeo, Grace Mkojera na Rahel Pallangyo, kutokana na kutambua mchango wao kwa kuripoti habari za mchezo huo.

Vyeti hivyo vilitolewa juzi na mgeni rasmi, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Luteni Jenerali Yakubu Hassan, baada ya kuhitimishwa kwa Mashindano ya Majeshi ya Afrika Mashariki.

Katika hatua nyingine, Mnadhimu huyo alisema atahakikisha anawapangia zamu majenerali kufanya mazoezi ya mchezo huo ili kushiriki kama ilivyo kwa nchi nyingine.

“Majenerali wa Malawi walikuja mwaka jana kushiriki mashindano ya majeshi na hapa kwetu Tanzania kuna haja kubwa ya kupangiwa ratiba ya kujifunza ili na sisi twende kwao tukashiriki,” alisema.

Jenerali Hassan alisema kwa sasa Tanzania hakuna majenerali wanaocheza gofu bali yakiwapo mashindano wengi wanaoshiriki ni wastaafu tofauti na nchi nyingine zinavyofanya.

Katika mashindano hayo ya siku mbili yaliyokuwa yamedhaminiwa na benki ya NMB, wengi walishinda kwa madaraja tofauti ila mshindi wa jumla alikuwa, Ally Mcharo, kutoka klabu ya TPC Moshi. Mnadhimu huyo aliwapongeza washindi wote kwa kujitahidi na kufanya kazi nzuri.

BAADA ya Yanga kurejea na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi