loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Omondi, MC Pilipili jukwaa moja

MCHEKESHAJI maarufu wa Afrika Mashariki, Erick Omondi (pichani juu), kutoka Kenya anatarajiwa kutua nchini na kufanya onesho la ‘Standup comedy’ katika jukwaa moja na mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’.

Onyesho hilo litafanyika Dodoma Septemba 28, mwaka huu, ambapo wakali hao watakutana kwenye jukwaa moja na kuonyesha nani zaidi.

Akizungumza na HabariLEO, Mc Pilipili alisema mchekeshaji Omondi amekuwa akimvutia tangu alipoanza kazi ya uchekeshaji na yeye ndio aliyemtia moyo katika kuingia kwenye fani hiyo baada ya kwenda kumuona katika moja ya maonyesho yake Nairobi.

“Nampenda sana Erick Omondi na anakuja Dodoma kufanya onyesha kali la uchekeshaji, naamini itagonga nyoyo za mashabiki wetu,” alisema. Pilipili alitaja kingilio katika onyesho hilo kubwa kuwa, viti maalum ‘V.I.P’ ni Sh 50,000 na Sh 30, 000, huku kawaida ikiwa Sh. 10,000.

Aidha aliongeza kuwa, mgeni rasmi katika tamasha hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Vijana, Ulemavu na Ajira, Anthony Mavunde, ambapo ataongozana na viongozi mbalimbali katika mkoa huo.

Pilipili alisema katika onyehso hilo anatarajiwa kusindikizwa na wachekeshaji wengine akiwamo Dullyvani, Dogo Pepe, Ally na Oscar Nyerere, huku wakiambatana na bendi ya TNC.

“Hii ni shoo yangu ya kwanza kufanya nikiwa nimeoa, mashabiki wangu mjitokeze kwa wingi muone kazi nitakayowaonesha na nitatoa nafasi tano kwa wachekeshaji wadogo wanaotokea Dodoma na viunga vyake kupanda stejini (jukwaani) na mimi na Omondi,” alisema Mc Pilipili.

BAADA ya Yanga kurejea na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi