loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mane aelezea furaha aliyo nayo Liverpool

SADIO Mane ameelekeza nguvu zake Liverpool, akisema “Napata tabu sana kuelezea nina furaha kiasi gani kuwa hapa.” Tetesi za uhamisho zimemuandama mshambuliaji huyo wa Senegal kwa muda mrefu, moja ya klabu zilizotajwa ni Real Madrid.

Tetesi zaidi zilizidi baada ya ushindi katika mechi ya Liverpool dhidi ya Burnley. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema anajisikia amani Merseyside. “Niwe mkweli, ninafuraha kuwa sehemu ya klabu hii, familia.

Tuna mashabiki bora duniani, kwa hiyo mara zote nafurahia sapoti.” “Si kwamba ni jambo jema tu kuwapo hapa, lakini inafanya kikosi kizima kiwe na hamasa, inatufanya tuwe na hasira ya kufanya vizuri zaidi na zaidi, napata shida sana kuelezea ni kiasi gani cha furaha ninacho kuwa nacho hapa,” alisema.

Mane amekuwa Liverpool kwa miaka mitatu mizuri, akifunga mabao 63 na kutwaa kiatu cha dhahabu kwenye Ligi Kuu na kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

ERIC Nshimiyimana amekubali mkataba mpya na sasa ataendelea kuwa Kocha ...

foto
Mwandishi: LIVERPOOL, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi