loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasanii wahamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura

KUNDI la wasanii wa uzalendo kwanza wamehimiza wananchi wa Kinondoni kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura ili kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa kundi hilo, Steven Mengele ‘Steve Nyerere ‘, alisema mchakato wa kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unatarajiwa kuanza Oktoba 8-14, mwaka huu.

Alisema wakazi wa Kinondoni wawe mfano kwa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi na kupata fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka wenye sifa zinazotakiwa na dhamira ya kweli kwa vijana.

“Leo tumekabidhiwa kanuni na sheria za uchaguzi kuhamasisha jamii ya Kinondoni kujiandikisha Daftari la Wapiga Kura na kushiriki uchaguzi, wanawake, vijana na wazee tujitokeze ili kuwa mfano mzuri kwa kujaza daftari, tuna ahidi kufanya kazi kwa weledi kwa kuwatoa pangoni waliojificha,” alisema.

Mengele aliyekuwa na kundi kubwa la wasanii wa muziki wa dansi, maigizo na bongo muvi na kizazi kipya, alisema taasisi yao itakuwa inaelimisha jamii ya manispaa hiyo kujiandikisha kwa kutumia burudani, lengo likiwa ni kuelimisha watu kushiriki kwa wingi katika uchaguzi.

Kwa upande wake, Katibu Msaidizi ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, alisema wao kama wana uzalendo wako tayari kuhamasisha kujiandikisha na kushiriki uchaguzi kupitia wimbo maalum watakaotunga.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi