loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magereza kujengwa kwenye wilaya 51

SERIKALI kupitia Jeshi la Magereza nchini ina mpango wa kujenga magereza katika wilaya 51 zisizo nayo kwa sasa. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusufu Masauni alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema) aliyetaka kujua mpango wa kujenga gereza katika kitongoji cha Nakato na kijiji cha Kibaoni wilayani Kilombero umefikia wapi.

Masauni alisema mpango wa kujenga magereza nchini utahusisha pia wilaya ya Kilombero ambayo ni miongoni mwa wilaya 51 nchini ambazo hazina magereza.

Aidha, mpango huo utatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa rasimali fedha. Alisema mpango wa kuwa na magereza katika kila wilaya, una lengo la kupunguza tatizo la msongamano kwenye baadhi ya magereza yanayopokea wahalifu kutoka wilaya zisizokuwa na magereza.

Masauni alisema mpango wa kuwa na magereza kila wilaya utarahisisha usikilizwaji wa kesi, wafungwa na mahabusu wataweza kupata huduma kwa urahisi kutoka kwa mawakili wao na pia kupunguza gharama za usafiri wa ndugu zao wanapowatembelea magerezani.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi