loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaigeria 600 kuondoshwa Afrika Kusini

TAKRIBANI raia 600 wa Naigeria wanatarajia kurudi nchini kwao kukimbia machafuko yanayotokana na chuki dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.

Balozi wa Nigeria nchini humo, Godwin Adama alisema raia watakaoondoka ni wale walioathiriwa na machafuko hayo tu. Alisema kuwa baadhi yao wataondoka leo kwa ndege mbili zilizoandaliwa, huku akiongeza kuwa ndege ya kwanza itaondoka na raia 320 na nyingine itafuata muda mfupi baadaye.

Msaidizi wa Raisi Muhammadu Buhari wa nchi hiyo, Bashir Ahmad alisema kuwa Raisi Buhari ametoa agizo la kurudishwa raia wote wa Naigeria walio tayari kurudi nyumbani kukimbia machafuko hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Diaspora wa Naigeria nchini Afrika Kusini, Abike Dabiri alisema kuwa Serikali ya Nigeria haitatoa fedha kwa ajili ya kurudisha raia hao, bali itahakikisha inaratibu shughuli yote na kuhakikisha wanafika salama ikiwa ni pamoja na kutoa vibali vya dharura kwa wale ambao pasipoti zao za kusafiria zimeisha muda wake.

“Serikali haitagharamia wanaorudi nyumbani ila itahakikisha inaratibu utaratibu mzima na kuhakikisha wanafika salama, pia itatoa vibali vya dharura kwa wale wote ambao pasipoti zao za kusafiria zimeisha muda wake,”alisema.

Dabiri pia aliomba Serikali ya Afrika Kusini kulipa fidia kwa raia wote walioathiriwa na machafuko hayo yaliyoanza mwanzoni mwa mwezi huu na kusababisa uharibifu wa mali na vifo.

Wakati huohuo, Serikali ya Naigeria imemtuma mjumbe maalumu, Ahmed Rufai Abubakr, kufaya mazungumzo na Raisi wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa kuhusu kadhia hiyo.

Ramaphosa amekiri kuwa machafuko hayo yameleta utata na ni fedheha. Kumekua na mfulululizo wa mauaji ya raia wa kigeni katika mji wa Johannesburg na maeneo jirani tangu wiki iliyopita, ikiwemo yale yaliyolengwa katika biashara na mali zinazomilikiwa na raia wa Naigeria.

Inaelezwa kuwa watu takribani 10 waliuwawa, mamia ya maduka yaliteketezwa na zaidi ya 420 walitiwa mbaroni. Machafuko hayo yalianza baada ya madereva wa malori kugoma wakipinga ajira za raia wa kigeni katika maeneo yao ya kazi na kuugwa mkono na raia wegine kabla ya kuchukua sura mpya ya mauji.

Afrika Kusini imekuwa kivutio kwa raia wengi wa kigeni kwa sababu ni nchi iliyoendelea zaidi katika bara la Afrika lakini nchi yenye ukosefu mkubwa wa ajira.

Kwa upande mwingine kituo cha radio maarufu cha Hot FM cha nchini Zambia kimepiga marufuku muziki wa wasanii wa Afrika Kusini katika vipindi vyake kama ishara ya kupinga mauaji hayo ya raia wa kigeni.

Meneja wa kituo hicho, Gary Masano alisema kuwa wanaoathirika katika mauaji hao ni pamoja na raia wa Zambia hivyo hawawezi kuendelea kuwaunga mkono wasanii wa Afika Kusini wakati wao wanawaua ndugu zao.

JUMUIYA ya Nchi za Afrika, Carribean na Pacifi c (OACPS) ...

foto
Mwandishi: PRETORIA, Afrika Kusini

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi