loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC ashukuru TIC kuwezesha uwekezaji Pwani

Mkuu wa Mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amekishukuru Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa namna kinavyoshirikiana na mkoa huo kuvutia wawekazaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya Serikali ya Awamu ya Tano kuiwezesha nchi kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda.

Amesema kwenye ofisi za kituo hicho jijini Dar es Salaam kuwa wamekuwa wakipata ushirikiano mkubwa kutoka watendaji wa TIC unaouwezesha mkoa huo kufanya vizuri katika viwanda.

“Mkoa wetu wa Pwani unafanya kazi karibu sana na taasisi zote wezeshi, TIC, Dawasa, NEMC, Brela, TBS, vyote pale.

Kwa mwekezaji anapokuja anapokuwa na changamoto kwa hiyo haoni tatizo sasa mpaka aende kwenye taasisi husika. Sisi kwa kushirikiana na taasisi ile tunajaribu kushirikiana ili kumpunguzia nenda rudi nenda rudi”amesema Mhandisi Ndikilo.

Amesema, mkoa huo kwa ufadhili wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF) umekamilisha mwongozo wa uwekezaji kwenye mkoa huo.

“Na mwongozo ule umeweka bayana kabisa fursa mbalimbali za uwekezaji katika mkoa wetu wa Pwani kuanzia masuala ya kilimo, masuala ya mifugo, masuala ya utalii, masuala ya uvuvi, na huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii”amesema.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, fursa hizo zitawekwa bayana kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi Oktoba tatu mwaka huu wakati wa Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Pwani.

JUMLA ya Dola za Marekani milioni 779 zimepatikana kutokana na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi