loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwili wa Mugabe waondoka Singapore, kuwasili leo Zimbabwe

Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe uko njiani kuelekea nchini huko kutokea nchini Singapore, taarifa zinaeleza.

Kiongozi huyo alikuwa akifanyiwa matibabu nchini Singapore kabla ya kukutwa na umauti Septemba 6, 2019.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha AFP, baada ya mwili kuwasili nchini humo, utapelekwa kijijini alikozaliwa Zvimba, Magharibi ya mji wa Harare kulaza msiba.

Alhamis na Ijumaa, mwili wa kiongozi huyo utawekwa kwenye Uwanja wa Mpira wa Rufaro, ambapo aliapishwa kwa mara ya kwanza kama Waziri Mkuu wa taifa hilo baada ya uhuru mwaka 1980.

Shughuli ya msiba wa kitaifa itafanyika rasmi Jumamosi, katika Uwanja wa Taifa wa nchi hiyo jijini Harare ambao kwa kawaida huweza kuchukua watu 60,000.

 

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: JANETH MESOMAPYA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi