loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchekeshaji 'Boss Martha' afariki, ujumbe wake gumzo

MCHEKESHAJI chipukizi Martha Shilole maarufu kama ‘Boss Martha’ amefariki dunia leo Jumatano asubuhi.

Akizungumza na HabariLeo, mchekeshaji mwenzake katika kundi la Cheka Tu, Lukinga Mkemwa ‘MC Lukinga’ amethibitisha kifo cha Martha na kueleza kuwa alikuwa anaumwa kwa takriban wiki tatu sasa.

Inaelezwa kwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kichwa, uti wa mgongo na malaria.

Mnamo Agosti 16, 2019 kwenye ukurasa wake wa Instagram, Martha alichapisha (aliposti) kupitia akaunti yake ya Instagram video ya mwanamuziki wa Injili wa nchini Malawi, James Nee aliyefariki kwa ajali Oktoba, 2018, na kuandika ujumbe unaosema ‘Oh Yesu, ukiniita jina langu, nitafurahi na kusema niko tayari kurudi nyumbani, na safari yangu hapa duniani ikiisha, nitafurahia na watakatifu nikiwa narudi nyumbani.”

Baada ya kifo chake, ujumbe huo ulioambatana na video umezua mijadala kwenye mtandao huo, wengi wakieleza kuwa huenda alifahamu kuwa atakufa.

Naye mwanzilishi wa Cheka Tu, Coy Mzungu kupitia ukurasa wake wa Instagram ‘ameposti’ picha akiwa na Martha wakati wa uhai wake na kufuatiwa na ujumbe unaosema, “Asante Mungu” na #MpenziwanguAmekwenda’.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: JANETH MESOMAPYA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi