loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwenyekiti Airtel Tanzania Dk Nundu afariki dunia

MWENYEKITI wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi yaAirtel Tanzania, Dk Omary Nundu, 71, amefariki dunia leo, Jumatano, Septemba 11, 2019.

Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kimethibitisha kifo hicho kupitia taarifa maalum kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Waziri huyo wa zamani alifikishwa hospitalini hapo akiwa kwenye gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki.

“Waliomleta waliamua kuhifadhi mwili wake katika hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo,” imeeleza taarifa hiyo.

Wakati wa uhai wake, Dk Nundu ameahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwa ni pamoja na kuwa mbunge wa Tanga na Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya awamu ya nne.

Aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania mnamo Juni 12, 2019 ili kusimamia utekelezaji wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi