loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC- Njooni mlime Bonde Mto Rufiji

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amesema, kuna fursa kubwa ya kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji maji kwenye Bonde la Mto Rufiji.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipoongoza ujumbe wa uongozi wa mkoa huo na timu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuzungumza na menejimenti ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Uongozi wa Mkoa wa Pwani umekwenda ofisi kuu za TADB kuona namna benki hiyo itakavyoshiriki kwenye Maonesho ya Pili ya Viwanda mkoani humo na Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mapema mwezi ujao.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, ushiriki wa benki hiyo utakuwa na tija kubwa kwao, kwa mkoa na nchi kwa ujumla.

Ndikilo amesema, kuna takribani hekta 150,000 kwenye Bonde la Mto Rufiji zinazofaa kwa kilimo cha miwa na ujenzi wa viwanda vya sukari, kilimo cha michikichi, kilimo cha mpunga, kilimo cha mahindi nk.

“Sasa maeneo yale kama tukiyanadi vizuri na TADB ikawa pia part and parcel ya mkoa wetu wa Pwani tunaweza tukapata uwekezaji mkubwa kabisa katika eneo la kilimo katika mkoa wetu lakini kwa nchi kwa ujumla”amesema.

Amesema, maonesho ya viwanda kwa wiki moja yanatarajiwa kushirikisha wenye viwanda takribani 500 kutoka mikoa minne ya kanda ya mashariki ukiwemo wa Tanga, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi