loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watu 100,000 kuona bidhaa za viwanda Pwani

Watu takribani 100,000 wanatarajiwa kutembelea maonesho ya viwanda mkoa wa Pwani mapema mwezi ujao.

Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Ndikilo amesema, maonesho hayo ya pili ya viwanda kwenye mkoa huo yatafanyika Oktoba Mosi hadi saba kwenye viwanja vya CCM Kibaha.

“Kwa hiyo ni namba kubwa, idadi kubwa ya watu ambao watafika pale, watapara taarifa mbalimbali lakini pia na kuona ambavyo taasisi mbalimbali namna zinaweza zikaonyesha maonyesho hayo” amesema.

Amesema jijini Dar es Salaam kuwa, mwaka jana wananchi 18,000 walitembelea maonesho hayo, na kwamba, ya mwaka huu yanatarajiwa kushirikisha wenye viwanda takribani 500 kutoka mikoa minne ya kanda ya mashariki ukiwemo wa Tanga, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

Amesema, hadi sasa Mkoa wa Pwani una jumla ya viwanda 1,192 vikiwemo vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo sana. Ametaja miongoni mwa maeneo yenye viwanda kuwa ni Rufiji, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Kibaha na Chalinze.

JUMLA ya Dola za Marekani milioni 779 zimepatikana kutokana na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi