loader
Picha

Shirika la ndege latoa tiketi 120 kwa CCBRT

Shirika la ndege la Precision Air limesaini mkataba wa ushirikiano na Hospitali ya CCBRT ili kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu nchini.

Kutokana na makubaliano hayo, shirika hilo litatoa tiketi za ndege 120 kwa hospitali hiyo kwa ajili ya kuwezesha shughuli zake za kliniki za matibabu mikoani pamoja na shughuli za kiutawala.

Akizungumza kwenye hafla ya kuweka saini mkataba huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Patrick Mwanri amesema ushirikiano huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za afya.

“Tunaelewa kwamba kuna vikwazo vingi vinavyozuia watu wanaoishi na ulemavu kusafiri kutoka mikoa mbalimbali kuja Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu, ndiyo maana tumashirikiana ili kwamba huduma hizi za kliniki ziwafikie huko waliko,” ameeleza.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa CCBRT, Brenda Msangi, asasi hiyo ina vituo washirika kwenye mikoa mbalimbali, hivyo watoa huduma wake wataweza kufikia watu wengi zaidi wenye uhitaji wa huduma kama za macho, mifupa, vipimo, ugawaji wa baiskeli kwa ajili ya walemavu na nyinginezo.

BAADA ya miaka miwili ya vuta nikuvute katika kesi ya ...

foto
Mwandishi: JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi