loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ufuta, korosho fursa ya utajiri Pwani

Korosho ni zao kuu la biashara mkoani Pwani, Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo amesema leo jijini Dar es Salaam.

Amesema katika msimu wa kilimo mwaka 2018/2019 mkoa huo ulikusanya tani 22,168 za korosho, na kwamba, zao hilo limekuwa likipandwa mwaka hadi mwaka na uzalishaji umekuwa ukiongezeka.

Ndikilo amesema kwenye ofisi kuu za Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Kinondoni kuwa, korosho zilizokusanywa zimewaingizia wananchi zaidi ya shilingi bilioni 60/-.

“Kwa hiyo nichukue fursa hii kwanza kuipongeza sana TADB…kwa hiyo benki ya TADB baada ya kupewa jukumu hili na Serikali imefanya kazi kubwa sana na mimi kwa niaba ya wananchi nikushukuru sana wewe (Mkurugenzi Mtendaji TADB) na wakurugenzi wako wote”amesema.

Amesema wananchi Pwani pia wanalima ufuta, na katika mwaka 2018/2019 wamekusanya tani 7,326 zilizowaingizia wakulima shilingi bilioni 21/-.

“Lakini zao lingine la biashara ni pamba, na pamba hii sana sana inazalishwa Chalinze, Kijiji Cha Miono, katika wilaya ya Bagamoyo.Na mwaka huu wamekusanya takribani tani thelathini za pamba”amesema.

JUMLA ya Dola za Marekani milioni 779 zimepatikana kutokana na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi