loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM amtembelea Askofu Ruwa’ichi, afanya maombi

RAIS John Magufuli amemtembelea na kumjulia hali Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Yuda Thaddeus Ruwa’ichi anayepatiwa matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)

Askofu Ruwa’ichi alianza kutibiwa mjini Moshi katika Hospitali ya KCMC kabla ya kupelekwa Muhimbili kwa ajili ya upasuaji wa kichwa.

Daktari mbobezi wa mishipa ya fahamu, Prof. Joseph Kahamba amesema kuwa hali ya Askofu Ruwa’ichi inaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji huo.

Akimjulia hali, Rais Magufuli ameungana na jopo la madaktari na wauguzi wa taasisi hiyo kumwombea Askofu Ruwa’ichi   afya yake izidi kuimarika ili aendelee na majukumu yake ya siku zote.

Akiwa katika chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalumu, Rais Magufuli amewatembelea wagonjwa mbalimbali waliofanyiwa upasuaji wa kichwa na kuridhika na utoaji wa huduma katika taasisi hiyo. Ambayo inatoa huduma kubwa za upasuaji ambazo hazikuwepo hapo awali ya uanzishwaji wake.

Prof Kahamba amemshukuru Rais kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika taasisi hiyo kwa miaka mitatu ikiwemo, ujenzi wa jengo,vitanda katika vyumba vya upasuaji na ICU, vifaa vipya vya uchunguzi, kama vile MRI, CT-Scan, X-ray ya kisasa,pamoja na ultrasound.

Hata hivyo, mkuu huyo wa nchi amewapongeza madaktari na wauguzi hospitalini kwa kazi kubwa wanayoifanya huku akiahidi kutoa 1.5bn / - kwa taasisi hiyo kununua viungo vya bandia kwa wagonjwa wanaoendelea kupokea matibabu hospitalini hapo.

Taarifa zaidi kuchapishwa katika gazeti la HabariLeo siku ya Alhamisi.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Ombeni Utembele

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi