loader
Picha

Viongozi 100 kumzika Mugabe

MWILI wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe umewasili Harare jana

Kuna mvutano kuhusu mahali atakapozikwa kiongozi huyo.

Watu mashuhuri na viongozi zaidi ya 100 wanatarajiwa kushiriki mazishi yake ya kitaifa yatakayofanyika keshokutwa.

Mugabe, mpigania uhuru wa Zimbabwe aliyetawala siasa za nchi hiyo kwa miaka 40 tangu ilipopata uhuru mwaka 1980, alifariki dunia Ijumaa ya wiki iliyopita nchini Singapore alikokwenda kwa matibabu.

Hata hivyo, mvutano umeibuka baina ya familia ya Mugabe na serikali ya nchi hiyo juu ya mahali atakapozikwa kiongozi huyo.

Familia yake inapinga mpango wa serikali wa kutaka mwili wake kuzikwa katika makaburi ya kumbukumbu ya mashujaa wa taifa jijini Harare badala yake inataka azikwe katika kijiji alichozaliwa cha Kutama.

Jana pikipiki za polisi zilisindikiza gari maalumu la kubebea maiti lenye rangi nyeupe aina ya Mercedes lililobeba mwili huo kutoka katika eneo ulipokuwa umehifadhiwa tangu alipofariki na kuelekea uwanja wa ndege, ambako muda mfupi baadaye uliingizwa katika ndege ambayo ilikuwa na baadhi ya maofisa wa serikali ya Zimbabwe akiwamo mpwa wake, Adam Molai.

Molai alisema ujumbe huo kutoka Zimbabwe uliwasili Singapore juzi na kuhudhuria misa binafsi ya kumwombea Mugabe katika Kanisa Katoliki iliyooongozwa na Padre kutoka Zimbabwe kabla ya kuondoka nao jana kurudi nao Zimbabwe.

Baada ya mwili huo kuwasili Zimbabwe jana, ulisafirishwa hadi katika kijiji cha Kutama alikozaliwa, Magharibi mwa Harare, ambako alikuwa akiheshimika kama shujaa.

Mwili huo utakesha hadi kesho ambapo utapelekwa Uwanja wa Rufaro unaochukua watu 35,000 mjini Harare ambako wananchi watatoa heshima zao za mwisho.

Uwanja huo ndiyo uliotumika kumuapisha Mugabekuwa Rais za Zimbabwe Aprili 18, 1980 baada ya kukabidhiwa madaraka na aliyekuwa waziri mkuu wakati wa utawala wa kikoloni, Ian Smith wakati nchi hiyo ikiitwa Rhodesia.

Mazishi ya kitaifa yatafanyika keshokutwa katika uwanja huo unaochukua watu 60,000 mjini ambapo viongozi wa mataifa mbalimbali wanatarajiwa kushiriki na mazishi rasmi yatafanyika Jumapili katika eneo ambalo hadi sasa ni kitendawili kutokana na mvutano uliopo na serikali.

Kwa mujibu wa Molai, mazishi ya kitaifa katika Uwanja wa Taifa yatahudhururiwa na marais kutoka mataifa mbalimbali wakiwamo wastaafu, watu mashuhuri na wananchi.

WATOTO yatima na wanaoishi kwenye mazingira wa magumu wa shule ...

foto
Mwandishi: HARARE, Zimbabwe

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi