loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Omary Nundu afariki dunia

MWENYEKITI wa Bodi ya Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania na aliyewahi kuwa Mbunge wa Tanga Mjini, Omary Nundu (71) amefariki dunia jana jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Nundu alifikishwa jana hospitalini hapo akitokea nyumbani kwa gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki.

Aidha, baada ya uchunguzi, waliompeleka hospitali waliamua wakahifadhi mwili wake katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lugalo pia jijini Dar es Salaam.

Juni 12, mwaka huu, Rais John Magufuli alimteua Nundu ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Uchukuzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu ya Airtel ikiwa ni makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Bharti Airtel International.

Kabla ya hapo, mbunge huyo wa zamani wa Tanga Mjini alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Mohamed Mtonga.

TTCL kwa upande wake ilithibitisha kifo hicho na kueleza kushtushwa na kifo cha Nundu aliyechaguliwa kuongoza Jimbo la Tanga Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi