loader
Picha

Zahera: Tunaijua Zesco ndani, nje

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema anajua udhaifu na uimara wa Zesco United ya Zambia, hivyo hana wasiwasi nayo.

Yanga Jumamosi itaikaribisha Zesco katika mchezo wa awali wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto Africans kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana juzi jijini hapa, Zahera aliwataka mashabiki wao wasiwe na wasiwasi watashinda mchezo huo wa keshokutwa.

Alisema anajua jinsi gani atakavyocheza dhidi ya Zesco United na aliwaambia wapenzi wa Yanga kuwa timu yao ilivyocheza mechi za kirafiki ni tofauti kabisa na itakavyocheza dhidi ya Zesco.

Alisema wapenzi wa timu hiyo wameiona Yanga ikicheza mechi za kirafiki dhidi ya Pamba na Toto Africans zote za Mwanza na kutoka sare ya 1-1 na kushinda 3-0 katika kambi yao ya Kanda ya Ziwa.

Alithibitisha kuwa mshambuliaji wao, Patrick Sibomana, atarejea nchini kwa ajili ya kucheza mchezo huo. Sibomana alikuwa ameenda kwenye timu yao ya Taifa ya Rwanda kwa ajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia.

Aliwaomba mashabiki wao waache tabia ya kuwazomea washambuliaji wao, Juma Balinya na David Molinga, kwani wanahitaji muda ili wafanye vizuri katika mechi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Zahera, Molinga alifunga mabao 25 katika Ligi Kuu ya Congo msimu ulioisha na Balinya alifunga mabao 25 katika Ligi Kuu ya Uganda, lakini anashangaa hapa nchini mashabiki wanawatukana.

Kwa upande wake, golikipa wa Yanga, Metacha Mnata, alisema watapambana kuifunga Zesco. Golikipa huyo wa zamani wa timu ya Mbao FC, Tanzania Prisons na Azam alisema anawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao katika michezo yao ya Ligi Kuu na ile ya kimataifa.

TIMU za Ligi Kuu Tanzania Bara zimegomea mfumo mpya unaotarajiwa ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi