loader
Picha

Samatta akunwa na Ndayiragije

NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na mshambuliaji wa klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, amefurahishwa na mbinu za Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije na kueleza zinawasaidia kuwa na ari ya kupambana uwanjani na kuahidi kufanya makubwa chini yake.

Samatta aliyasema hayo alipokuwa kambini na Taifa Stars katika michezo miwili ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia, ambapo walifanikiwa kufuzu hatua ya makundi baada ya kuifunga Burundi kwa panalti 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa baada ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa awali uliochezwa Burundi.

“Ndoto kubwa ninayoiota kwa sasa ni siku moja kuja kucheza michuano ya Kombe la Dunia, japo matumaini ya kufikia hatua hiyo kuna ugumu hivyo tunatakiwa kupambana,” alisema Samatta.

Kuhusu michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu, Samatta alisema kwake ni jambo kubwa kupata nafasi ya kucheza katika Uwanja wa Anfield unaomilikiwa na klabu ya Liverpool kwa kuwa ni klabu kubwa, lakini alipendelea zaidi kama wangepangwa kundi moja na Barcelona au Real Madrid za Hispania.

“Unaposhiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya huwezi kukosa kukutana na vigogo kama hao, mabingwa wa nchi mbalimbali.

Lakini ningependa zaidi kukutama ama na Barcelona au Real Madrid, ila hata hivyo Anfield pia ni moja ya sehemu bora sana, si mbaya kucheza na timu kama Liverpool na Napoli,” alisema.

Samatta anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, ambapo katika kundi la Genk kuna timu za Liverpool, Napoli na Salzburg.

Pia atacheza kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Uingereza pindi atakapovaana na Liverpool katika dimba la Anfield.

KOCHA wa timu ya soka ya wanawake ya Tanzania chini ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi