loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtibwa yapania kuimaliza Simba

KOCHA msaidizi wa Mtibwa Sugar, Patrick Mwangata, amesema anataka kuweka historia yake mpya kwa kuhakikisha anaifunga Simba katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mwangata amepewa nafasi ya kukiongoza kikosi hicho baada ya Kocha Mkuu, Zuberi Katwila, kupewa jukumu la kuingoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes.

Akizungumzia mchezo huo jana, alisema Simba ni timu nzuri, lakini haimaanishi kuwa hawaihofii, bali wanajipanga kwa kutumia vijana wao kupata matokeo mazuri.

“Mchezo wetu wa Simba tunajua hautakuwa rahisi kwasababu wako nyumbani mbele ya mashabiki wao watapambana kupata matokeo, lakini na sisi pia tunahitaji matokeo, tumejipanga kuwakabili,” alisema.

Alisema jukumu alilopewa sio dogo hivyo ni lazima atengeneze kikosi chake kwa kutumia vijana wengi alionao kupata ushindi.

Kwa upande wake, msemaji wa klabu hiyo yenye makazi yake Morogoro, Thobias Kifaru, alisema mchezo huo utawakosa nyota watatu, ambao ni Shaban Nditi ambaye ni majeruhi, huku Juma Luizio na Jaffar Kibaya wakiwa Misri kwenye majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Mtibwa Sugar ilianza mchezo wa kwanza wa ligi vibaya baada ya kupoteza ugenini dhidi ya Lipuli kwa kipigo cha mabao 3-1. Kwa upande wa Simba, Kocha Mkuu, Patrick Aussems, alisema bado ana hofu kuelekea mchezo huo baada ya mshambuliaji wake, Meddie Kagere, kuumia akiwa na timu yake ya taifa ya Rwanda.

Alisema Kagere ni mshambuliaji pekee aliyekuwa anamtegemea baada ya John Bocco kuumia, hivyo sasa atalazimika kumuandaa Mbrazil Wilker Da Silver ambaye ametoka kupona majeruhi.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi