loader
Picha

Ronaldo afunga manne Ureno ikishinda

CRISTIANO Ronaldo alifunga mabao manne wakati Ureno ikiifunga Lithuania 5-1, katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2020.

Mshambulia huyo wa timu ya Juventus, sasa amefunga mabao 93 katika mechi za kimataifa, ikiwa ni mabao 16 nyuma ya gwiji wa Iran, Ali Daei anayeshikilia rekodi ya dunia.

Nyota huyo alifunga bao la mapema kwa penalti, kabla Vytautas Andriuskevicius hajasawazisha. Shuti la Ronaldo kutoka meta 20 lilipita juu ya kichwa cha kipa wa Lithuania, Ernestas Setkus na kufunga mabao mengine mawili zaidi baada ya kupata pasi ya Bernardo Silva, kabla William Carvalho hajafunga la tano katika dakika za mwisho.

Matokeo hayo yanaifanya Ureno kufuzu moja kwa moja, ikiwa pointi tano nyuma ya vinara wa Kundi B Ukraine. Hiyo ni hat-trick ya nane katika mechi ya kimataifa kwa Ronaldo, ambaye sasa ana umri wa miaka 34, ambaye pia alifunga mabao manne walipocheza dhidi ya Andorra mwaka 2016.

Serbia ilipanda hadi katika nafasi ya tatu katika kundi hilo baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Luxembourg, huku Aleksandar Mitrovic akizifumania nyavu mara mbili.

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema ...

foto
Mwandishi: LISBON, Ureno

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi