loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TADB yatangaza neema kilimo cha mahindi

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inaziona fursa za biashara na uwekezaji mkoani Pwani na inaamini itakuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika kuzitumia.

Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Japhet Justine ametaja miongoni mwa fursa zitakazotumika Pwani ni kuongeza thamani ya zao la mahindi.

Ameyasema hayo Dar es Salaam wakati menejimenti ya TADB ilipozungumza na ujumbe wa uongozi wa mkoa wa Pwani akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Ndikilo na timu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Justine amesema bodi ya TADB imeidhinisha utekelezaji wa mradi mkubwa wa kujenga kiwanda cha kusaga mahindi, na kwamba, sehemu ya mradi huo ipo Mbozi lakini kiwanda kikubwa kinajengwa Kibaha, Pwani.

“Kwa hiyo tunaamini kwenye value chain, kwenye mnyororo wa thamani wa mahindi at leat tumeshaweka mnunuzi kwa hiyo sasa ni kurudi nyuma kuhamasisha”amesema.

Kwa mujibu wa Justine, Tanzania tatizo si uzalisha ila masoko hivyo kupitia mradi huo unaofanyiwa kazi sasa, mahindi yatakuwa biashara kwa kuwa TADB inafungua fursa kwenye zao hilo.

“Mabadiliko makubwa ya kilimo yanafanyika au inabidi yafanyike kwa kumgusa mkulima mmoja mmoja pale tunapokwenda chini na kukutana na mkulima na kumsikiliza na kutoka pale kuangalia tunawezaje kufanya kazi nae hivyo sasa unaweza ukasema umefanya mabadiliko”amesema

JUMLA ya Dola za Marekani milioni 779 zimepatikana kutokana na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi