loader
Picha

Zafuzu makundi Kombe la Dunia Afrika

MECHI za mwisho za raundi ya kwanza ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022 kwa bara la Afrika zilikamilika juzi Jumanne.

Hatua hiyo ya raundi ya kwanza ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2022, ilishiriisha jumla ya mataifa 28, ambayo yako chini katika viwango vya soka barani Afrika.

Timu 14 zilizopata ushindi wa jumla katika mechi mbili za nyumbani na ugenini, zitaungana na zingine 26, ambazo ziko katika viwango vya juu, zenyewe hazikucheza raundi hiyo ya kwanza ya mchujo.

Raundi ya pili Kwa mujibu wa utaratibu, raundi ya pili ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022, itakuwa ni hatua ya makundi na itashirikisha jumla ya mataifa 40, ambayo yatapangwa katika makundi 10, yenye timu nne kila moja kusaka nafasi ya kucheza play-off.

Kila kundi litatoa timu moja ya kwanza, yaani mshindi wa kundi hilo atatinga hatua ya play-off, ambapo timu hizo 10 zitapangiwa ratiba na kila timu itacheza na mpinzani wake mmoja, mechi ya nyumbani na ugenini ili kumpata ushindi, ambaye moja kwa moja atafuzu kwenda Qatar 2022.

Mechi za juzi Malawi, Djibouti na Zimbabwe zote zilishinda mechi zao kwa tofauti ya bao moja dhidi ya Botswana, Eswatini na Somalia, ikikamilisha hatua hiyo ya raundi ya kwanza ya kufuzu na kutinga hatua ya makundi.

Timu zingine kama Msumbiji, Angola, Togo, Rwanda, Guinea-Bissau, Namibia na Sudan zilikuwa na kazi nyepesi ya kutinga raundi ya pili.

Rwanda wenyewe ndio waliweka rekodi baada ya kuichapa Shelisheli kwa jumla ya mabao 10-0, pia ilikuwa jioni ya kihistoria kwa Guinea-Bissau.

Walifuzu kwa mara ya kwansza raundi ya pili , baada ya kuifunga Sao Tome e Principe 2-1 katika mchezo wa marudiano. Zilizofuzu mapema Kabla ya mechi hizo za Jumanne, tayari timu nne zilikuwa zimeshafuzu kwa hatua hiyo ya makundi baada ya kucheza mechi zao za marudiano Jumapili, ikiwemo Tanzania, Liberia, Ethiopia na Guinea ya Ikweta.

Timu hizo nne ndizo zilikuwa za kwanza kupenya kutoka katika hatua hiyo ya mtoano, ambayo ilishirikisha jumla ya timu 28. Ratiba kamili Hatua hiyo ya makundi ya kusaka nafasi ya kucheza play-off itaanza kupigwa Machi 2020.

Matokeo yote ya Jumanne: Eswatini vs Djibouti 0 – 0 (1 – 2 Jjibout ilipata ushindi wa jumla) Malawi vs Botswana 1 – 0 (1 – 0 Malawi imepenya) Zimbabwe vs Somalia 3 – 1 (3 – 2 Zimbabwe imepita) Msumbiji vs Mauritius 2 – 0 (3 – 0 Msumbiji ilipenya) Angola vs Gambia 2 – 1 (3 – 1 Angola ilifuzu) Rwanda vs Seychelles 7 – 0 (10 – 0 Rwanda imefuzu) Sudan vs Chad 0 – 0 (3 – 1 Sudan imefuzu) Togo vs Comoros 2 – 0 (3 – 1 Togo imepita) Guinea-Bissau vs Sao Tome e Principe 2 – 1 (3 – 1 Guinea ilipita) Namibia vs Eritrea 2 – 0 (4 – 1 Namibia imepita) Nchi ambazo zimefuzu hatua ya makundi:

Ethiopia, Tanzania, Guinea ya Ikweta, Liberia, Malawi, Zimbabwe, Djibouti, Msumbiji, Angola, Togo, Rwanda, Guinea-Bissau, Sudan na Namibia. Fainali za 22 za Kombe la Dunia, ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Waarabu, zinatarajia kuanza Novemba 21, 2022. Fainali itapigwa Desemba 18, 2022, ambayo itakuwa ni siku ya taifa ya nchi hiyo.

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema ...

foto
Mwandishi: CAIRO,Misri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi