loader
Picha

Kijaji: Idadi ya watu ni fursa kiuchumi

UTAFITI wa idadi ya watu duniani unaonesha idadi ya watu ni fursa ya nguvu kazi kwa nchi, iwapo mambo muhimu matano au baadhi yake yatafanyika, Bunge limeelezwa.

Hivyo serikali imejielekeza zaidi katika kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na kufanya biashara na hivyo kutumia ongezeko la idadi ya watu kama fursa ya nguvu kazi ya kuzalisha mali pamoja na soko la bidhaa na huduma.

Hayo yalisemwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bunda Vijijini, Boniface Getere (CCM) aliyetaka kujua mikakati ya serikali kudhibiti kasi ya ongezeko la idadi ya watu.

Alitaja mambo hayo kuwa ni kuboresha maisha ya watoto na kuboresha elimu na uwezeshaji kwa wanawake, kuimarisha uwekezaji katika afya ili kuwa na nguvu kazi bora na yenye tija.

Aidha, alitaja jambo jingine kuwa ni kuimarisha uwekezaji katika elimu ya juu ili kuwa na nguvu kazi yenye elimu, ujuzi na ubunifu, huku akitaja kufanya mageuzi ya kiuchumi yanayolenga kuharakisha ukuaji wa uchumi na upatikanaji wa kazi kwa ajili ya nguvu kazi iliyopo kuwa ni jambo la nne na jingine likiwa ni mageuzi ya sera ili kuvutia wawekezaji wa kigeni na kuhakikisha uwajibikaji hasa katika rasilimali za umma.

Kijaji alisema, dhima ya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2017 - 2020/2021 ni kujenga uchumi wa viwanda ili kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu.

Alisema mpango huo umejikita zaidi katika uwekezaji wa kimkakati kwenye sekta ya viwanda, kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, kusambaza umeme mijini na vijijini na kusambaza pembejeo za kilimo kwa wakati.

Alisema pia umejikita katika kutatua changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa kujenga bwawa kubwa la kufua umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji, kuimarisha huduma za jamii kwa kujenga na kukarabati miundombinu ya maji, hospitali na vituo vya afya vya umma, shule pamoja na kutekeleza kwa ufanisi sera ya elimu bila malipo.

WATOTO yatima na wanaoishi kwenye mazingira wa magumu wa shule ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza, Dodoma

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi